Mwanza: Baba amuua binti yake kutokana na kuchelewa kurudi nyumbani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Baba mmoja anayefahamika kwa jina la Anthony Maningu, Mkazi wa Kayenze wilayani Ilemela mkoani Mwanza kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga na kitu kizito kichwani mwanaye aitwae Veronica Anthony, kwa madai ya kuchelewa kurudi nyumbani.

Akizungumza hii leo Septemba 10, 2020, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Muliro Jumanne, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema Baba huyo yupo chini ya ulinzi na uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea, na mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

Katika tukio lingine, Kamanda Muliro amesema katika Kata ya Shibula wilayani Ilemela, Emmanuel Joseph mwenye umri wa miaka 49, aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito utosini na ndugu yake aitwae Mussa Gabriel, baada ya kumtuhumu kumuibia simu yake yenye thamani ya Shilingi elfu Arobaini.
 
Huyo mzee atakuwa alikuwa anamtafuna mwanae.
Kama unazaa utaelewa wanao wakishakuwa wakubwa,kuna hii situation unajikuta unasomesha shule mtoto kwa gharama kubwa ukiamini unamuandalia maisha yake ya baadae ila unakuta hakuna anachokielewa zaidi Bodaboda mtaani wanamgombania na ukimkanya hakanyiki.

Sidhani kama mzazi nia yake ilikuwa amuuwe mwanae hapo ilikuwa ni zile adhabu za kawaida za kila siku ila ndo ilishapangwa litokee na limetokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Baba mmoja anayefahamika kwa jina la Anthony Maningu, Mkazi wa Kayenze wilayani Ilemela mkoani Mwanza kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga na kitu kizito kichwani mwanaye aitwae Veronica Anthony, kwa madai ya kuchelewa kurudi nyumbani.

Akizungumza hii leo Septemba 10, 2020, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Muliro Jumanne, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema Baba huyo yupo chini ya ulinzi na uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea, na mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

Katika tukio lingine, Kamanda Muliro amesema katika Kata ya Shibula wilayani Ilemela, Emmanuel Joseph mwenye umri wa miaka 49, aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito utosini na ndugu yake aitwae Mussa Gabriel, baada ya kumtuhumu kumuibia simu yake yenye thamani ya Shilingi elfu Arobaini.
Hapo kanda ya ziwa haya ni kawaida. Inasikitisha.
 
Labda alikuwa anategemea kupokea mahari kubwa kwenye posa ya mwanae. Kakosa kila kitu.
 
Back
Top Bottom