Katika kile kilichoonekana kuwashangaza wengi, ni kuingiliana na kukaribiana kwa mikutano miwili ya kampeni ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na chama cha ACT Wazalendo.
Tukio hilo limetokea Novemba 26, 2024, Mtaa Isamilo, kata Isamilo, Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa ACT ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa ACT bara, Ester Thomas.