Pre GE2025 Mwanza: CV za Wabunge 2020 - 2025. Mbunge wako ametimiza ahadi zake?

Pre GE2025 Mwanza: CV za Wabunge 2020 - 2025. Mbunge wako ametimiza ahadi zake?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakuu,

Eric Shigongo - MBUNGE WA BUCHOSA

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kura: 20,581
Mpinzani: Mwambino Julius Isack (CHADEMA) – 11,285
Elimu: Shahada ya Uhusiano wa Umma (Public Relations) kutoka Tumaini University (2020)
Biashara: Mmiliki wa Global Publishers Ltd, Global Radio Ltd, Global Television Ltd, na Bwemark Real Estate Ltd

Kazi ya Kisiasa:
Aliingia Bungeni mwaka 2020
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira (2021–2023)




2. Angeline Sylvester Lubala - MBUNGE WA ILEMELA

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kura: 147,724
Mpinzani: Grayson Wanzagi Warioba (CHADEMA) – 24,022

Elimu:
Master’s Degrees katika Community and Economic Development (2014)
Public Administration and Business Management (2019)

Uzoefu wa Kazi:
Mhasibu
Koordineta wa Kitengo cha Jinsia na Maendeleo cha Caritas Mwanza
Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala wa Mkoa wa Mwanza

Kazi ya Kisiasa:
Mbunge wa Ilemela tangu 2020
Naibu Waziri katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (2016–2020)




3. Mansoor Shanif Jamal - MBUNGE WA KWIMBA

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kura: 57,943
Mpinzani: Josephat Bonephace Kayanda (CUF) – 1,917

Elimu: Shahada ya Uhandisi ya Umeme kutoka Tanesco Institute (1997)

Biashara: Mkurugenzi Mtendaji wa Mansoor Industries Ltd

Kazi ya Kisiasa:
Mbunge wa Kwimba
Kamati la Kilimo, Mifugo na Maji
Kamati ya Bajeti ya Bunge
Kamati ya Miundombinu




4. Kiswaga Boniventura Destery - MBUNGE WA MAGU

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kura: 139,975
Mpinzani: Ndindagi Reginald Kwizela (CHADEMA) – 14,479

Elimu: Astashahada ya Uongozi na Utawala wa Fedha kutoka Chuo cha Uongozi Kijitonyama

Kazi ya Kisiasa:
Mbunge wa Magu
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (2012–2017)
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (2003–2008)

Biashara: Mkurugenzi wa Lugeye Investment na Lugeye Oil




5. Stanslaus Mabula - MBUNGE WA NYAMAGANA

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kura: 73,591
Mpinzani: Pambalu John Justine (CHADEMA) – 42,209

Elimu: Shahada ya Uzamili katika Uongozi kutoka Chuo Kikuu cha Mysore, India

Kazi ya Kisiasa:
Mbunge wa Nyashimo
Meya wa Manispaa ya Mwanza (2012–2015)

Kazi za CCM:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM
Katibu Mkuu wa UVCCM Mwanza




6. Tabasamu Hamisi Hussein - MBUNGE WA SENGEREMA

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kura: 59,734
Mpinzani: Victoria Benedict Tindabatangile (CHADEMA) – 7,949

Elimu: Shule ya Msingi Nyakato

Kazi za Kisiasa:
Diwani wa Sengerema
Mbunge wa Sengerema
Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge

Uongozi wa CCM:
Diwani na Mbunge wa Sengerema




7. Kasalali Emmanuel Mageni - MBUNGE WA SUMVE

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kura: 31,373
Mpinzani: Sangalali Shija Masanja (CHADEMA) – 6,285

Elimu: Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma

Kazi za Kisiasa:

Diwani wa Lyoma Street
Mbunge wa Sumve
Kamati ya Sheria za Kiutawala

Kazi za CCM:
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Mwanza (2018–2020)




8. Joseph Mkundi - MBUNGE WA UKEREWE

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kura: 91,893
Mpinzani: Sijaona James Karoli (CHADEMA) – 23,361

Elimu:
Shahada ya Uongozi wa Biashara (BBA) kutoka St. Augustine University
MBA kutoka Open University of Tanzania

Kazi za Kisiasa:

Mbunge wa Ukerewe
Kamati ya Masuala ya Nje, Ulinzi, na Usalama ya Bunge
Naibu Waziri Kivuli wa TAMISEMI (2015–2018)
 
Baadhi elimu ni ya hapa na pale
Ukona matu amaonyesha kuwa ana Masters au ana shahada, bila kuweka chronologically alifikia elimu hiyo vipi, basi ujue ni ya kuunga. Au mtu anamaliza darasa la 7 tuseme mwaka 1995 halafuu baada ya hapo amna elimu yoyote aliyopata bali alipata shahada ya uzaamili mwaka 2020 (yaani baada ya miaka 15), basi ujue shahada hiyo ni ya magumashi.
 
Hivi Angeline Mabula si ndo Waziri kamili wa hiyo wizara.?
Huyo anakurupuka kuandika, eti Stanislaus Mabula alikuwa meya wa manispaa ya 2012-15, hakuna manispaa ya Mwanza huo mwaka huyo jamaa alikuwa meya wa jiji.
 
Back
Top Bottom