Mwanza: Hili Dampo la Buhongwa ni chanzo cha Magonjwa ya Tumbo na Kipindupindu

Mwanza: Hili Dampo la Buhongwa ni chanzo cha Magonjwa ya Tumbo na Kipindupindu

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Dampo la Buhongwa lipo eneo la Manispaa ya Nyamagana Jiji Mwanza, rekodi za Serikalini zinaonesha lilijengwa kwa gharama ya shilingi Milioni 8.87.

Licha ya ukubwa wa Dampo hilo ambalo awali wakati linajengwa Mwaka 2020 lilisifiwa kuwa ni sehemu sahihi ya kuhifadhi taka lakini mambo yamebadilika sana ndani ya muda mfupi kutokana na uchafu uliokithiri eneo hilo.

Kutokana na uchafu kuzidi eneo hilo kuna wakati mamlaka zinazohusika zilianza kumwaga kemikali fulani kwa lengo la kukata harufu na mara kadhaa kutumia kemikali hizo kuchoma taka lakini hilo halijasaidia.

Kinachotia shaka zaidi ni kuwa karibu na dampo hilo kuna soko maarufu kwa jina la Soko la Dampo, hivyo usalama wa dampo unapoyumba inamaanisha kiafya pia sio salama.
Dampo (1).png

Dampo (5).jpg
Katika dampo hilo na maeneo yote ya jirani kuna harufu kali na mbaya ambayo imesababisha wengi wetu tuwe tunaumwa vifua, matumbo ikiwemo kuharisha.

Magari ya taka yanayofika hapo kumwaga yanamwaga kiholela, ni kama kila mtu anafanya anavyojua yeye, hakuna utaratibu wa kueleweka.

Mvua zinaponyesha hali inakuwa mbaya kuliko maelezo, uchafu unasambaa na hata vile vyakula vinavyouzwa katika soko lililopo jirani na Dampo navyo sio salama kiafya.

UUZWAJI WA MCHANGA

Dampo (2).JPG


Kuna kikundi cha Watu kinafanyabiashara ya kuuza mchanga eneo hilo la kwa ndani na inapotokea wanajua kuna Kiongozi anaenda eneo hilo, wanachofanya ni kuziba mashimo yaliyochibwa kwa kuweka mbolewa zinazozalishwa humo inamaanisha wanaziba mashimo.

Pia ukionekana tu unafika eneo hilo kwa ukaribu maswali yanakuwa mengi unakwenda wapi na mengineyo hii inaleta taswira hasi ya kile kuinachoendelea kwenye dampo hilo.

Hii tabia haijazungumzwa kwa wingi lakini inaweza kuwa chanzo cha kuharibu mazingira zaidi na zaidi.
cce552f1a966e689c63790613f005b0a.jpeg
Kemikali zinaumiza Watu
Mbali na hapo uchomaji taka unapokuwa unafanyika hasa kwa kuwa unahusisha nia ya kupunguza harufu kali, moto unachukua muda mrefu kuzima, moshi unakuwa ni kero na athari kubwa kwetu.

Vyoo havitumiki inavyotakiwa
Licha ya kuwa kuna vyoo lakini baadhi ya Watu katika Soko la Dampo wamekuwa wakijisaidia sehemu ambazo sio rasmi, ukijumlisha na uwepo wa Dampo na hizo changamoto zake kinachotokea ni uharibifu mkubwa wa usafi wa mazingira.

Pamoja na yote hayo kumekuwa na ahadi nyingi za viongozi kuhusu maboresho ya Dampo hilo lakini hakuna kinachofanyika cha maana.

PICHA ZIKIONESHA UJENZI WA DAMPO ULIVYOKUWA
101661273_2499493123634270_2490478245904908288_n.jpg

102662966_2499493020300947_9119888197176786944_n.jpg
 
Ila aliyetoa wazo la kuhamishia soko karibu na damponsijui aliwaza nini
 
Hivi viongozi wa haya maeneo wanashinda kwa ahadi zipi?(Msiniletee habari za kura zinaibwa!)

Wananchi mjipende, hii nchi ni yenu pia. Jambo dogo kama hilo ni la kuhakikisha viongozi wenu wanalisolve ndani ya muda mchache.

Afya ni kitu muhimu sana, acheni kujichukia.
 
Back
Top Bottom