Mwanza: Luhaga Mpina na Hussein Bashe uso kwa uso kwenye mkutano wa hadhara

Mwanza: Luhaga Mpina na Hussein Bashe uso kwa uso kwenye mkutano wa hadhara

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Screenshot_20240913_174219_Facebook.jpg
MWANZA; Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amekutana na Mbunge wa Jimbo la Kisesa, wilayani Meatu Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina kwenye mkutano unaoendelea katika Mji wa Mwandoya Jimbo la Kisesa.

Juzi akiwa wilayani Igunga mkoani Tabora, Waziri Bashe, alisema atafanya ziara katika Jimbo la Mbunge huyo na kuzungumza na wananchi, lengo ni kuwauliza kama wanahitaji serikali iendelee kuwapatia huduma za pembejeo na ugani.

Bashe alisema kuwa Mbunge huyo amekuwa akitoa tuhuma kwa serikali juu ya huduma hizo kuwa hazina ubora, lakini wanunuzi wa pamba wamekuwa wakiwaibia wakulima.

Leo Septemba 13, 2024, Waziri Bashe amezungunza na wananchi wa jimbo hilo, katika mkutano wa hadhara unaofanyika katika Kijiji cha Mwandoya, mkutano ambao Mpina amehudhuria.

Imeandaliwa na Derick Milton

Pia, soma:
 
Back
Top Bottom