Mwanza: Maji yaanza kutoka Buhongwa. Ni baada ya Waziri Aweso kuweka Kambi na Mafundi Site

Mwanza: Maji yaanza kutoka Buhongwa. Ni baada ya Waziri Aweso kuweka Kambi na Mafundi Site

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
AWESO AKAMILISHA KAZI YA WIKI KWA SIKU 1 BUHONGWA,KAZI YAKAMILIKA USIKU

AWESO AKAMILISHA KAZI YA WIKI KWA SIKU 1 BUHONGWA,KAZI YAKAMILIKA USIKU

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amehakikisha Kazi iliotakiwa kufanyika ndani ya wiki moja ya ukamilishaji wa Mradi wa Maji wa Buhongwa jijini Mwanza ilitokiwa kukamilishwa mpaka ijumaa inafanyika ndani ya siku moja kwa kuamua kuweka kambi na mafundi site mpaka saa sita usiku.
Mradi wa dharula Buhongwa umekamilika usiku na Maji rasmi yamefika hapa Buhongwa Centre na kazi itakayofuata ni kuunganisha kwa wananchi.

Awali Waziri Aweso ameshuhidia maunganisho ya bomba ya mwisho ya mradi wa Sahwa Buhongwa ambao unalenga kutatua changamoto katika maeneo ya Sahwa, Lwanhima na Buhongwa.

Mara baada ya bomba la mwisho kuunganishwa saa 4.15 usiku alielekea katika kituo cha kusukuma maji Sahwa ili kuwasha pump ya maji kwa lengo la kusafisha bomba hilo.

Usiku huo huo Waziri Aweso amewakabidhi wenyeviti wa serikali za mitaa za Sahwa chini na Semba mabomba kwa ajili ya kusogeza maji katika maeneo yao.

Mradi huu una gharama ya Tshs. Milioni 864.816. Mradi huu utanufaisha wakazi wa mitaa ya Sahwa ya chini, Sahwa ya juu, Buhongwa mashariki, Buhongwa magharibi, Buhongwa centre na Maliza.
Jumla ya vituo nane vya kuchota maji vitajengwa katika maeneo hayo na kunufaisha wananchi katika mitaa husika.

Pia, soma:
 
Nimepita hapo usagara naskia matangazo kuwa awesu yupo...ila ni jambo la fedheha sanaa kuona lipo km kama mbili tu afu watu wanakosa maji
 
TANESCO bado wako na usingizi wa "porno''...
Wala hawashtuki kuiga mfano wa Juma
 
Hongera kwao, Waziri oyeeee

Miezi miwili na baada ya wadau kurusha humu ametekeleza.

Hii inaonyesha uzembe wa makusudi wa Watendaji kazi wa serikalini, na biashara ya kuuza maji.

Watasaka njia ingine kula vya kupanga, mazoea mabaya sana hayo yaliyojaa tamaa na urefu wa kamba ukiwa umewanogea.
 
CCM Wajanja sana ktk mbinu za kisiasa
Ni aibu hadi leo suala la maji bado ni tatizo
yaan wanang"ata na kupuliza
huyo waziri asiishie ktk mradi moja maana ipo miradi haijakamilika
 
CCM Wajanja sana ktk mbinu za kisiasa
Ni aibu hadi leo suala la maji bado ni tatizo
yaan wanang"ata na kupuliza
huyo waziri asiishie ktk mradi moja maana ipo miradi haijakamilika
 
Back
Top Bottom