A
Dah!Wazubae hivyohivyo kama udaga.Wataendelea kwenda kuoga ziwani uchi hadharani kama watu wasiostaarabika hadi dahari.Wananch wa MZA tulieni - mama anaupiga mwingi, kesho yatatoka mengi muoge hadi mtambae.
Mlivyoambiwa mkaandamane mbona hamkutokea, pambaneni na CCM yenu.Wakazi wa mbezi huku mageti na maeneo ya karibu kama muhimbili wamemkosea nini mama mwezi Wa pili hawana maji eti ni sababu za kisiasa
Kwani mpaka leo maji ni kero huko Mwanza?Haya ndiyo mambo ya kuungana wote na kuandamana bila kujali vyama .
Maji ni uhai .
Serikali yoyote isiyoweza kutoa huduma ya maji kwa wananchi wake ni serikali isiyojali uhai wa watu wake .
Wanakimbilia miradi ya kitapeli lakini miradi ya maji yanayotokana na mito ,maziwa na hata kujenga mabwawa kwa ajili ya uhai wa wananchi inasuasua na kuifanya iwe ni sehemu ya kampeni za kisiasa .
Nilishangaa juzi Mama mkubwa akizindua mradi wa maji wa kule Kilimanjaro .
Ule mradi ulianza kwenye kampeni za mwaka 2010 . Mbunge wa wilaya ya Mwanga wakati huo Profesa Maghembe akapewa mpaka Wizara ya maji . Wananchi wakiaminishwa kuwa Kufikia 2015 maji yatakuwa kama mafuriko wilaya za Mwanga na Same. 2015 kampeni za uongo zinaendelea maji yakiwa agenda .2020 zinaendelea ,maji yakawa ni agenda . Sasa ni 2025 ,maji kwenye majimbo hayo bado ni agenda .
Maji ni uhai ,serikali haijali uhai wa wananchi wake.
Wanaharakati na wanasiasa wapo kimya wanasubiri maandamano ya kudai tume huru peke yake . CCM inapata kiburi cha kuendelea kuwahadaa wananchi kuwa wao wanaahidi maji sio katiba kwani maji ndiyo maendeleao wanayotaka kusikia wananchi na sio katiba .
Kwa hiyo ni vyema sasa wanaharakati wahalasishe maandamano ya wananchi kudai huduma muhimu kama maji ambayo ni muhimu kwa uhai wa viumbe vyote ili CCM ikose pa kujificha na kuhadaa watu .