Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza kwa matukio matatu tofauti likiwemo la vijana wawili ambao ni makada wa CHADEMA kukamatwa wakiwa na karatasi 181 za kupigia kura.
Kamanda wa Polisi Kamishina Msaidizi wa polisi DCP Wilbroad Mutafungwa, amesema majira ya saa moja na nusu asubuhi katika kituo cha kupigia kura cha Lwanhima B, mtaa wa Maliza ambapo vijana hao ambao ni mawakala wa Chadema, Edward Otieno na mgombea wa uenyekiti wa mtaa huo Athanasi Ndaki walichukua boksi ambalo lilikuwa na karatasi za kupigia kura na kuondoka nazo.
"Mgombea huyo kwa kushirikiana na wakala huyo walichukua karatasi hizo na kuondoka nazo lakini kabla hawajafika mbali askari waliokuwa kwenye eneo hilo walifanikiwa kuwakamata na baada ya kufanya uchunguzi walibani wagombea hao wakiwa na karatasi zingine zilizokuwa zipigiwa kura," amesema DCP Mutafungwa
Tukio lingine ni wakala wa kituo cha Lwanhima A , Ally Hussein ambaye naye anashikiliwa kwa kosa la kukimbia na karatasi za kupigia kura 181 zikiwa zimehifadhiwa. " Watuhumiwa hao wanashikiliwa na uchunguzi unaendelea,"Amesema DCP Mutafungwa
DCP Mutafungwa pia amesema wanamshikilia Amos Ntobi ambaye ni katibu wa Chadema wilaya ya Nyamagana kwa kosa la kufanya fujo kwenye kituo cha kupigia kura cha Kabengwe mtaa wa Mabatini akidai kuwa kituo hicho kutokuwepo kwenye orodha ya kupigia kura.
PIA SOMA
- LGE2024 - Mwanza: Nane mbaroni kwa kukimbia na kura za mwenyekiti