Dr. Wansegamila
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 2,968
- 8,139
Kutoka mkoani Mwanza Jeshi la Polisi inamshikilia Zawadi Msagaja (20) na wenzake wawili akiwemo mganga wa kienyeji, kwa tuhuma za kumzika mtoto wake mwenye umri wa miezi miwili akiwa hai, kwa lengo la kumtoa kafara ili apate utajiri.
Watuhumiwa wengine ni dada yake Zawadi, Elizabeth Kaswa na mganga wa kienyeji, Mussa Mazuri.
Tukio hilo lilitokea Novemba 13, mwaka huu, katika Mtaa wa Kisundi, Kata ya Bugogwa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mganga huyo alimpa Zawadi maagizo ya kutekeleza kitendo hicho, huku akimtishia asipofanya hivyo angemtoa yeye kafara.
"Mwanamke huyo alikuwa akiishi kwa dada yake, alifanya unyama huo baada ya kutishwa na mganga wa kienyeji ambaye ni shemeji yake Mussa James Mazuri (31), amtoe kafara mtoto wake wa kike Neema Claud mwenye umri wa miezi miwili, wote watatu wapate utajiri, endapo angekataa angemtoa yeye kafara." amesema Kamanda Mutafungwa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.