Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
WanaJF,
Mada hii itakuwa na 'Updates' za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Mwanza. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kushiriki na wengineMkoa wa Mwanza ni moja ya mikoa muhimu nchini Tanzania, ukiwa katikati ya Kanda ya Ziwa na ukipakana na Ziwa Victoria. Ni mkoa wa pili kwa idadi ya watu baada ya Dar es Salaam na ni kitovu cha biashara, usafiri, na uchumi wa Kanda ya Ziwa.
MUHTASARI WA MAENEO YA UTAWALA, MKOA WA MWANZA
Katika muhtasari wa maeneo ya utawala, mkoa huu una halmashauri ambazo zimegawanyika katika mamlaka za miji na wilaya.
1. Idadi ya Watu
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022, Mkoa wa Mwanza una jumla ya watu wapatao 3,690,499.SOMA PIA: Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
2. Wilaya za Mkoa wa Mwanza
Mkoa wa Mwanza una jumla ya wilaya 8, ambazo ni:- Ilemela (Halmashauri ya Manispaa)
- Nyamagana (Halmashauri ya Jiji)
- Magu
- Misungwi
- Kwimba
- Sengerema
- Ukerewe
- Buchosa
3. Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi
Mwanza ina jumla ya majimbo 9 ya uchaguzi:- Jimbo la Nyamagana
- Jimbo la Ilemela
- Jimbo la Magu
- Jimbo la Misungwi
- Jimbo la Kwimba
- Jimbo la Sengerema
- Jimbo la Buchosa
- Jimbo la Ukerewe
- Jimbo la Sumve