Pre GE2025 Mwanza: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pre GE2025 Mwanza: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

WanaJF,​

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Matukio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Mwanza. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

Mwanza.jpg

Mkoa wa Mwanza ni moja ya mikoa muhimu nchini Tanzania, ukiwa katikati ya Kanda ya Ziwa na ukipakana na Ziwa Victoria. Ni mkoa wa pili kwa idadi ya watu baada ya Dar es Salaam na ni kitovu cha biashara, usafiri, na uchumi wa Kanda ya Ziwa.

MUHTASARI WA MAENEO YA UTAWALA, MKOA WA MWANZA
Katika muhtasari wa maeneo ya utawala, mkoa huu una halmashauri ambazo zimegawanyika katika mamlaka za miji na wilaya.

Idadi ya Watu

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa na idadi ya watu katika Mkoa wa Mwanza ni 3,699,872; wanaume 1,802,183 na wanawake 1,897,689 ikiwa na walaya 8.

Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi

Mwanza ina jumla ya majimbo 9 ya uchaguzi:
  • Jimbo la Nyamagana
  • Jimbo la Ilemela
  • Jimbo la Magu
  • Jimbo la Misungwi
  • Jimbo la Kwimba
  • Jimbo la Sengerema
  • Jimbo la Buchosa
  • Jimbo la Ukerewe
  • Jimbo la Sumve
HALI YA UCHAGUZI MKUU 2020

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, Mkoa wa Mwanza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilifanikiwa kushinda kwa wingi katika ngazi zote.

Katika uchaguzi wa rais, Hayati John Magufuli wa CCM alipata kura nyingi zaidi mkoani Mwanza, huku wagombea wa upinzani wakipata kura chache kwa ujumla.

Kwa upande wa ubunge, CCM ilishinda majimbo yote ya mkoa huo, na mgombea mmoja alishinda bila kupingwa katika jimbo la Misungwi.

Kwa ngazi ya udiwani, CCM ilipata viti 189 kati ya kata 191 zilizopo mkoani Mwanza, huku kata mbili tu zikichukuliwa na CHADEMA katika jimbo la Sumve

Updates

January
February
March


ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
 
Back
Top Bottom