LGE2024 Mwanza: Mgombea ADC alalamika vipeperushi vyake kubanduliwa na kubandikwa vya CCM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mgombea Uenyekiti wa Mtaa wa Nela Kata ya Isamilo jijini Mwanza kwa tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), James Dioniz, amelalamikia kitendo cha vipeperushi vyake kubanduliwa, kisha kubandikwa vya mgombea Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abubakar Seif.

Akizungumza na Mwananchi leo, Jumatatu, Novemba 25, 2024, Dioniz amesema Jumamosi Novemba 23, alibandika vipeperushi vyake maeneo mbalimbali ya mtaa huo ikiwemo kwenye mbao na nguzo, ili kunadi sera na vipaumbele vyake, lakini siku moja baadaye alikuta baadhi ya vipeperushi hivyo vimechanwa na vingine vikiwa vimefunikwa na vipeperushi vya mshindani wake wa CCM.

Alipotafutwa na Mwananchi Digital kwa njia ya simu, Mgombea wa CCM, Abubakar Seif amesema tuhuma za mgombea huyo wa ADC zinalenga kumchafua kisiasa na kutafuta kiki, huku akidokeza ukomavu alionao kwenye siasa kwa zaidi ya miaka 30 hana haja ya kubandua vipeperushi hivyo.

Akizungumzia sakata hilo, Ofisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Lilian Masha, amesema ofisi yake haijapokea malalamiko rasmi kwa mgombea wa ADC.

Amesema Kifungu cha 6.4.1 (vi) kinakataza chama cha siasa kuchafua, kubandua, kuchoma au kuharibu kwa namna yoyote ile matangazo ya kampeni ya vyama vingine vya siasa.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - LGE2024 - Dodoma: Wapiga Kura wakiwa na Vipeperushi vya mwenyekiti wa CCM Wakati wa Kujiandikisha
 
Kungekuwa na umoja huu uonevu ungeisha, sasa kila mmoja analalamika kivyake, chadema inaandamwa sana ila vyama vyote kimya wanasubiri mpaka waguswe wao.
umoja wa walalamikaji au umoja wa makambale gebtleman? :pulpTRAVOLTA:
 
Mgombea Uenyekiti wa Mtaa wa Nela Kata ya Isamilo jijini Mwanza kwa tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), James Dioniz, amelalamikia kitendo cha vipeperushi vyake kubanduliwa, kisha kubandikwa vya mgombea Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abubakar Seif.

Akizungumza na Mwananchi leo, Jumatatu, Novemba 25, 2024, Dioniz amesema Jumamosi Novemba 23, alibandika vipeperushi vyake maeneo mbalimbali ya mtaa huo ikiwemo kwenye mbao na nguzo, ili kunadi sera na vipaumbele vyake, lakini siku moja baadaye alikuta baadhi ya vipeperushi hivyo vimechanwa na vingine vikiwa vimefunikwa na vipeperushi vya mshindani wake wa CCM.

Alipotafutwa na Mwananchi Digital kwa njia ya simu, Mgombea wa CCM, Abubakar Seif amesema tuhuma za mgombea huyo wa ADC zinalenga kumchafua kisiasa na kutafuta kiki, huku akidokeza ukomavu alionao kwenye siasa kwa zaidi ya miaka 30 hana haja ya kubandua vipeperushi hivyo.

Akizungumzia sakata hilo, Ofisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Lilian Masha, amesema ofisi yake haijapokea malalamiko rasmi kwa mgombea wa ADC.

Amesema Kifungu cha 6.4.1 (vi) kinakataza chama cha siasa kuchafua, kubandua, kuchoma au kuharibu kwa namna yoyote ile matangazo ya kampeni ya vyama vingine vya siasa.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - LGE2024 - Dodoma: Wapiga Kura wakiwa na Vipeperushi vya mwenyekiti wa CCM Wakati wa Kujiandikisha
amefanya vizuri sana kulalamikia mitandaoni,
huenda akapata kuhurimiwa na wana mitandao:pulpTRAVOLTA:
 
ADC ni chama rafiki na ccm. Queen Sendiga, RC wa Manyara alikuwa mgombea urais kupitia chama hiki.

Haya ni malalamiko shikizi ili ionekane kuwa vyama vyote vinafanyiwa hujuma kama chadema.
 
Back
Top Bottom