Tetesi: Mwanza: Mkuu wa Chuo ‘Atekwa’, Apotea

Tetesi: Mwanza: Mkuu wa Chuo ‘Atekwa’, Apotea

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
018 by Global Publishers

polisi-2.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna ameeleza juu ya tukio la kupotea kwa Mkuu wa Chuo cha Nyakato Islamic Institute kilichopo chini ya Taasisi ya Elimu ya The Registered Trustees of Islamic, Sheikh Bashir Gora na kudai jeshi linaendelea kumtafuta.



Kamanda Shanna amesema ni kweli wamepokea taarifa za kupotea kwa Sheikh huyo hivyo ameagiza kufungwa kwa mipaka yote ya Mkoa wa Mwanza ili kuhakikisha kiongozi huyo anapatikana mapema iwezekanavyo.



“Ni kweli tumezipata taarifa za kupotea kwake, lakini unajua mtu akipotea huwezi kujua tatizo ni nini, na hatujui kwanini hapatikani na tumemtafuta kila mahali hapatikani, tumeshafunga mitambo yetu kwenye maeneo yetu yote.”



Akizungumza hivi karibuni, Katibu wa Bodi wa taasisi hiyo, Sadik Mchola alisema tukio hilo lilitokea Desemba 6 chuoni hapo ambapo alikuja kijana mmoja kuulizia nafasi za kujiunga na chuo kwaajili ya mdogo wake.



“Kijana huyo alitukuta ofisini, Sheikh akamwambia aje Januari mwakani atapewa utaratibu, kijana aliondoka lakini baada ya muda kidogo akarudi tena kuulizia malipo, Sheikh akamwambia Januari ndiyo tutakueleza kila kitu, akaondoka.”



“Baada ya hapo wakawa wanazungumza na Sheikh huku anamsindikiza kumbe walikuwa wameegesha gari yao nyuma ya chuo walipoikaribia, alitoka kijana mwingine kwenye gari hiyo wakambeba Sheikh na kumuingiza ndani kisha gari likaondoka kwa speed (mwendo) mkali,” alisimulia.
 
Naona huu umekuwa muendelezo wiki Kama mbili zilizopita kuna Sheikh Mkubwa mkoani Tanga naye alitekwa na kupelekwa pasipo julikana baada ya kufuatiliwa kituoni polisi walikana kutokuwa na taarifa zozote lakini mwisho wa siku ikaja kujulikana kuwa alitekwa na watu wa Usalama
 
Inaitwa mbwa kala mbwa...!

Mnyeeezi mungu amnusur mja wake dhidi ya maswahibu yote...walakin zaidi akamhepushe na adhabu ya kabr wasije mtenda yaliyo mabaya.

Takibiiir.....!


Wabillah Tawfiq
 
Back
Top Bottom