Mwanza mshikaji wenu nimetia mguu, nipeni ramani

Mwanza mshikaji wenu nimetia mguu, nipeni ramani

navigator msomi

Senior Member
Joined
May 8, 2018
Posts
188
Reaction score
224
Wadau kama nilivokwisha kutoa habari hapo kabla ya kuwa na nia ya kuja kuishi mwanza, hatimae nimetimba kibabe takribani zinakatika wiki mbili...

Kwasasa niko maeneo ya Buhongwa Nyamagana ila cha ajabu mpaka saizi sijaona inshu gani nifanye ili niweze ingiza mia mbili tatu.

Kuanzia asubuhi mpaka saa saba nina kibarua hua nafanya kinachoniingizia kipato fulani,ila lengo langu nataka ongeza kipato kwa njia nyingine hasa muda ambao ninakua free kuanzia saa nane.

Mtaji nilionao mpaka saizi cash in hand ni 10ml lakini nataka nipate inshu ambayo haitozidi 1m ili niweze masta mazingira kwanza then baadae ndio naweza jilipua mtaji mkubwa..

Naombeni wadau mnipe direction hasa kwa wenyeji wa Mwanza kipi kinaweza nipatia hata ka faida ka buku tano kila sikuuu asanteeeeni
 
Nenda Sahara sokoni tafuta sehemu ya kupata kinywaji taratibu huku ukichunguza mishe mishe za soko asubuhi hadi jioni, utapata mishe ya kufanya kwa hiyo 1 million
 
Kuna mdau alileta uzi wa mtu kuwa usijenge nyumba nunua mtumbwi usome na ule pia
 
Nenda buhongwa sokoni pale ulizia bei ya nyanya wanauzaje kwa cret ukipata jibu sema nikuunganishe na mtu mwe mnapeleka rwanda na uganda mzigo wenu.

hii biashara haihitaji masharobaro mkuu kuna muda utakuwa unazifata vijijini kwa wakulima na ndo zina faida mno
 
Hapo Buhongwa mbona pamechangamka, fanya kujiongeza.
 
Kwa jinsi palivochangamka buhongwa, we nenda kachukue samaki wabichi mswahili ama kirumba. Unatafuta friji ya kutunzia hao samaki.
Hapo unauza samaki wabichi na WA kukaangwa. Mwanza ni walaji wa samaki sana. Mbona utauza sana mkuu
 
Back
Top Bottom