RESOLVED Mwanza: Taka zilizorundikwa Stendi ya Makoroboi zimeondolewa

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
​
Siku kadhaa zilizopita (Juni 23, 2026) niliandika kuhusu mazingira ya katika stendi ya mabasi madogo ya Makoroboi jijini Mwanza kuwa na uchafu mwingi.

Nilieleza uchafu huo umekuwa ukitoa harufu kali kwa siku siku kadhaa na kuwa kero kwa Wananchi na watumiaji wa eneo hilo.

Hali ilivyokuwa awali ~ Mwanza: Taka zilizorundikwa Stendi ya Makoroboi zinanuka sana, ni hatari kwa Afya zetu

Nafurahi kuona baada ya andiko hilo hatua zimechukuliwa na uchafu umeondolewa, kwani mazingira kweli hayakuwa mazuri na kulihitajika hatua za haraka, sababu uchafu kama huo ni mwanzo wa maambukizi ya magonjwa hasa ya tumbo.
​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…