KERO Mwanza: Uchafu unaotolewa kwenye mifereji Barabara ya Bwiru-Kitangiri na kuachwa muda mrefu, unapunguza ukubwa wa barabara

KERO Mwanza: Uchafu unaotolewa kwenye mifereji Barabara ya Bwiru-Kitangiri na kuachwa muda mrefu, unapunguza ukubwa wa barabara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mwanangikolo

Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
63
Reaction score
105
Moja kwa moja kwenye mada!

Kuna muda mpaka unajiuliza hivi huu mkoa kweli una viongozi au ni vile wako bize na timu yao ya Pamba Jiji.

Barabara ya Kona ya Bwiru kuelekea Kitangiri na inayounga mpaka Bwiru, pembezoni mwa barabara kumejaa uchafu unaotolewa kwenye mifereji ya barabara hiyo.

Uchafu unakaa mpaka mwezi mzima bila kuzolewa hali inayosababisha mpaka barabara kuwa finyu na watembea kwa miguu kujikuta wanatembea katikati ya barabara kitu kinachofanya kuweka usalama wao hatarini na pia kuchafua mazingira kwa kuchafua muonekano wa Jiji.

Juzi kidogo mama mmoja agongwe na gari baada ya kujikuta anatembelea usawa wa katikati ya barabara baada ya kuwa anakwepa kupita kwenye uchafu huo unaorundikwa pembezoni mwa barabara hiyo, na kero hii ipo sana kuanzia lilipo Kanisa la Baptist mpaka ilipo Baa ya ZE DREAM na Hoteli ya TOURIST.

Viongozi mlioaminiwa na Rais shughulikieni hili suala maana mnafanya mpaka Wananchi lawama zao kwenda mpaka kwa Rais, hivi serious kweli kuzoa uchafu mpaka kauli itoke Ikulu?

Nina imani ujumbe umefika au Wazungu wanasema "message delivery".
IMG_20250214_122849.jpg
 
Back
Top Bottom