KERO Mwanza: Wakazi wa Buhongwa hatuna maji ya uhakika, hufunguliwa usiku wa manane

KERO Mwanza: Wakazi wa Buhongwa hatuna maji ya uhakika, hufunguliwa usiku wa manane

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
BUHONGWA KAMA JANGWANI
Wakazi wa Buhongwa jijini Mwanza hatuna maji ya uhakika. Kutoka vyanzo visivyo rasmi inasadikika wafanyakazi wa idara ya maji wana miradi yao ya kuuza maji ambapo hukata maji kwa makusudi na kuyafungulia nyakati za usiku waweze kujaza matenki yao na kisha kuyauza kwa wakazi kwa bei wanayoitaka wao.

Kwa fikra za kawaida tu majukumu ya kazi huisha saa 12 jioni, sasa huyu anayefungua maji saa kumi au saa nane usiku ni mfanyakazi wa aina gani?
download.jpeg
 
Buhongwa,Nyashish hakuna maji
Waziri mkuu alisema linajengwa Tank kubwa labda ndio wanasubiria yakhee sijui yatafika Nyashish maana ushakuwa mji mkubwa
 
Karibu nyamongoro mkuu huku yanafunguliwa satisa na nusu usiku mpaka sakumi kasoro dk5 yanasepa😂 kitu kngne mkuu nimependa hlo bamba lilivyo😂😂
 
Back
Top Bottom