Watoto wawili wanafunzi wa Shule ya Blessing Model School iliyoko Nyasaka Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wametekwa na watu wasiojulikana huku wengine wane wakinusurika.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea siku ya Jumatano tarehe 5 Februari, 2025 muda wa saa 12 asubuhi eneo la Kapriponti jijini Mwanza baada ya mtu asiyejulikana kuomba lifti kwenye gari la shule hiyo lililokuwa na wanafunzi sita.
Kamanda Mutafungwa amesema mtu huyo baada ya kupanda kwenye gari na kutembea umbali kidogo alimkaba dereva akitokea upande wa nyuma kisha kuwabeba watoto wawili na kuondoka nao kupitia usafiri wa pikipiki mbili zilizofika eneo hilo muda mfupi baada ya kutokea tukio hilo.
Mutafungwa amesema chanzo cha tukio hilo ni tamaa ya fedha kwani watekaji wameanza kutuma ujumbe wa simu na vitisho kwenye uongozi wa shule wakiwataka watoe fedha ili kuwapata watoto hao.