Mwanzo-Mwisho: Mhadhara wa Kiprofesa na Profesa Rwekaza Mukandala

Mwanzo-Mwisho: Mhadhara wa Kiprofesa na Profesa Rwekaza Mukandala

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
21 May 2024

Mwanzo - Mwisho: Mhadhara wa Kiprofesa na Profesa Rwekaza Mukandala

Mhadhara wa Kiprofesa kuhusu dola , Masoko, na Kufeli kwa Kitaasisi : Mafunzo toka Kuletwa duniani kwa lazima (kuzaliwa kwa mzazi kulazimishwa uchungu uje) , Maisha ya Kuteseka na Kifo cha Uchungu cha MV. Bukoba


View: https://m.youtube.com/watch?v=vuJYR2JCLLQ

Mbele ya wageni maarufu kama Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, jaji mkuu mstaafu Chande na wengine wengi .. .

Mafunzo kutoka katika kujifungua kwa uchungu wa kushinikiza, maisha ya mateso, na kifo cha maumivu cha MV. Bukoba. Prof. Rwekaza Sympho Mukandala PhD (UC Berkeley), MA (UDSM), BA (UDSM), profesa wa Sayansi ya Siasa na Utawala, Profesa wa Kigoda cha Mwalimu J. K. Nyerere katika Taaluma za Umajumui wa Afrika (Pan africanism), na Makamu Mkuu wa Chuo Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam UDSM ....

Profesa Mukandala leo Jumanne Mei 21, 2024 akitoa muhadhara wa kiprofesa UDSM ikiwa ni miaka 28 tangu meli MV Victoria izame jijini Mwanza.

Katika maelezo yake, amesema meli hiyo ilifanya kazi miaka 17 nchini pasina kusajiliwa na wala haikupaswa kuletwa nchini.

Katika utangulizi profesa Palamagamba Kabudi akielezea wasifu wa Prof. Rwekaza Sympho Mukandala PhD ..... toka viti jalalani hadi kukaa katiika viti vya karibu na mfalme rejea biblia Zaburi 13 ......tukio la leo siyo kitu cha kawaida kukumbuka ajali iliyotokea tarehe 27 May 1996 ziwa Victoria ...

Professorial Inaugural Lecture​

21.May.2024 11.03

Professorial Inaugural Lecture on States, Markets, and Institutional Failure: Lessons from the Induced Birth, Tortured Life, and Painful Death of MV. Bukoba

This is to inform the University of Dar es Salaam community and the general public that Prof. Rwekaza Sympho Mukandala, from the Department of Political Science and Public Administration, College of Social Sciences (CoSS), will deliver his Professorial Inaugural Lecture on States, Markets, and Institutional Failure: Lessons from the Induced Birth, Tortured Life, and Painful Death of MV. Bukoba on Tuesday 21st May 2024 from 14:00hours at Nkrumah Hall, University of Dar es Salaam.

Prof. Mukandala is a dedicated scholar, researcher, educator and leader working particularly in the areas of Public Administration, Comparative Politics, and Democratic Governance.

His professorial inaugural lecture will be delivered on the 28th anniversary of the sinking of MV. Bukoba. Commissioned on 27th July 1979 by President Julius Kambarage Nyerere, she started her last voyage from Bukoba Port on 20th May, 1996. She capsized between 07:35 and 07:40 am on 21st May as she approached the Gulf of Mwanza and eventually sank at 15:05 pm on the same day.

According to H.E. Benjamin William Mkapa, Third President of the United Republic of Tanzania it was at that time the worst tragedy to happen in the country's history. Conflicting claims and counter claims abound regarding the cause of the accident.

Prof. Mukandala deploys a multi-disciplinary historical approach, ranging from physics to political science, law and economics, to explore the key contributory factors to what it is concluded was the induced birth, tortured life and painful death of MV. Bukoba.

Finally, important lessons are drawn for the present and future .... READ MORE : University of Dar es Salaam-
 

Jenerali Ulimwengu Apigilia Msumari Suala la Katiba Mbele ya Maprofesa; 'Waliokanyaga Mchakato Wako


View: https://m.youtube.com/watch?v=vxXJnbrN6n4

Jenerali Ulimwengu awapa tano Maprofesa, kutukumbusha tulipotoka ikiwemo katiba mpya ili kupunguza madaraka ya mtu aliye mfano wa imperial presidency / rais mfalme. Ikiwa tuna baraza la mawaziri magarasa ambao hawasikilizwi na rais ni bora tuwe na ufalme usio na baraza la mawaziri wala bunge ili kupunguza gharama za uendeshaji serikali ... nampongeza Prof. Rwekaza Sympho Mukandala PhD kwa muhadhara huu wa leo ulio wa kipekee anamalizia Jenerali Ulimwengu
 
Huu ulikuwa zaidi ya mhadhara wa Uprofesa " inaugural lecture" ni magisterial inaugural lecture. Umepiga mulemule na umetumia lugha maridhawa ya Kiswahili yaani full raha ni kuelewa kila nukta hata kama hutaki.

Profesa Rwekaza Sympho Mukandala ametutendea haki wavuvi wa mwalo wa Kemondo.
 
Mhadhara wa Kiprofesa kuhusu dola , Masoko, na Kufeli kwa Kitaasisi :

21 May 2024
JENERETA la HOSPITALI HALIJAFANYA KAZI MWAKA MZIMA - KISA KUKOSA MKAA - CHUMVI - DIZEL - RC AWAKA...

View: https://m.youtube.com/watch?v=lMiUzRRmGic

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda ameshangazwa kukuta genereta la Hopsitali ya Wilaya ya Busega mkoani humo ambalo lilitolewa na Wizara ya Afya likiwa halijatumika kwa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na kukosa vifaa vya majaribio ambavyo baadhi yake ni kilo tano za chumvi, makopo mawili ya mkaa, pamoja na lita 15 za Disel.Katika ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya jana Hospitalini hapo, Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa mbali na hivyo, vitu vingine ni nyaya mbalimbali ambapo awali watalaamu walileta bajeti ya zaidi ya Sh Milioni 20 kwa ajili ya kununua ....
 
Mhadhara wa Kiprofesa kuhusu dola , Masoko, na Kufeli kwa Kitaasisi :
21 May 2024
WAZIRI MCHENGERWA AKASIRIKA ATOA MIEZI 2 MKURUGENZI KUKAMILISHA UJENZI HOSPITALI IFAKARA...

View: https://m.youtube.com/watch?v=xvP-0l3baBE

Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI mh Mohamed Mchengelwa ametoa miez miwili kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji ifakari, Zahara Michuzi kuhakikisha ujenzi wa hospital ya wilaya unakamilika ndani ya miezi hiyo miwili kutokana na kusuasua kwa ujenzi wa hospital hiyo.

Huku chanzo kikiwa ni ugomvi Kati ya wanasiasa na viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia, Waziri mchengelwa anatoa maagizo hayo Wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na hapa ni katika hospitali ya wilaya ya mji ifakara inayojengwa katika kata ya kibelege na imeshindwa kukamilika kwa wakati kutokana na mivutano ya kisiasa ....
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=mrHNfoOyung

Profesa Mukandala anaeleza kuwa pamoja na rasimu ya Katiba kutoa mapendekezo ya kutaka Rais kufuata ushauri au kutoa maelezo kwenye baraza la mawaziri asipofuata ushauri, Katika Bunge la Katiba mabadiliko hayo yaliondolewaAkikamilisha muhadhara huo, Mukandala amesisitiza ili kuboresha dola, lazima Tanzania iangalie upya Katiba ......
 
Back
Top Bottom