Mwanzo wa binadamu, maswali ni mengi kuliko majibu!

Wote mnaobeza biochemical evolution theory ni wale ambao mlipata bahati mbaya ya kutofundishwa vizuri ktk maada ya EVOLUTION na mwalimu wako aliishia kukuambia binadamu chanzo chake ni nyani au kama ulifundishwa vizuri bhaasi ulokole wako ndio tatizo.

Tuliofundishwa vizuri tulielezwa msingi wa Evoluti ni kwamba viumbe hai hubadilika kutoka form rahisi (simple) kwenda form tata (complex) kwa kadiri unavyo kwenda.

Msingi wa evolution ni kwamba mabadiliko haya hutokea ndani ya miaka mingi eg 10,000yrs ili uweze kunote changes zilizopo sina maana kwamba miaka hiyo ijayo binadam atakuwa kiumbe mwingine ila kimwonekano miaka hiyo ijayo kunaweza kuwafanya wawe na shape tofauti na sisi vile hata uwezo wa ubongo wao utakuwa mkubwa kiasi kwamba vifaa vyote bora vilivyotengezwa leo ungepata kuwepo ungelivicheka sana.

Hapa nimekujibu unaepasua kichwa kujiuliza kwa nini nyani wa leo hawawi binadamu, au kwa nini binadamu wa leo habadiliki tena? Ujue kwamba umri wako wa kuishi duniani hautoshi kugundua mabadiliko ktk wakati uliopo, ili wengine wanotice changes ni mpaka vizazi hivyo vipotee.

Na kingine ni kwamba binadamu huwa na interest inayo sumbua wao hivyo binadamu hatuna interest na history background ya nyani, mbwa, paka etc kuwa na record ya evolution but in general we keep knowing they undergone changes over the course of time.

Si kweli kwamba chanzo cha binadamu ni nyani au sokwe ila tulifundishwa ktk hatua za mabadiliko alipitia hatua ambayo alifanana na sokwe wa leo, kwa maana alitembea kwa miguu minne lakini alikuwa na nywele za mwilini nyingi na mfumo wake wa chakula ulifanana na hao viumbe. Labda uliza wakati huo Sokwe wa leo walikuaje?

Tunachoamini ni kwamba viumbe wote tumetoka ktk cell moja ya kwanza na cell hiyo ndio imeefanya evolution kwa mechanism kama ilivyo fafanuliwa na Charles Darwin.

Labda na maswali haya ungeweza kujiuliza na upande wa special creation theory, nadharia ya MUNGU.

1. Kuna MUNGU wangapi?
2. Ikiwa kama tuaminvyo ni super natural mmoja, kwa nini haikufanyi ufikiri huyo naye ana MUNGU wake mwenye uwezo mkubwa kuliko wake na ndio aliyemuumba huyu tumjuaye?
3. Huyo Adam na Hawa (Eva) walikuwa ni watu gani wazungu, waarabu, wachina au Waafrika? Je hizi haina tofauti za watu zimetokeaje kutoka kwa watu hao wawili?

Upungufu wako utajibu si kwa fikra zako bali kwa maandishi walioandika wenzako katika dini yako.
 
Noted

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We mtu hujui chochote kuhusu mungu wala huelew chochote kuhusu mwanadamu wewe na Darwin ni walewale thats why umemeza idea zake japo uez ata kuzidadavua.

Katika hali ya uumbaji hakuna mwenye jibu ila katika hali ya mungu mimi nina jibu maana kwa macho, masikio, na fahamu zangu nimekuwa nikimuexperience mungu katika power flani kubwa nikiwa namuomba yeye power design ya shoti ya umeme ambayo huingia mwilini mwangu na hii hunifanya kuogopa sana kupuuza chochote anachoongelewa mungu katika kitabu chochote na pia hii power hunifanya niamini nadharia yoyote ya mwanadamu kupitia theology basi ni ya kweli maana ina be proved na natural power ambazo ideology hizi inazizungumzia na tunaziexperience the way nlivyokueleza apo so acha emagination na umake proof kutushawish.
 
Ukweli wa jibu sahihi na ujasiri ni hili, kuhusu huyo adamu na eva sijui na kuhusu evolution siamini kwa mana nyani wapo kibao hadi nyani ngabu, ah sorry nyani babu yupo na habadiliki mpaka wakati wa kifo chake. Sasa tuishi kwa wakati wetu wa kufa na kuzaliwa ila na sisi maisha yetu yatakuwa ni history ya miaka ya 3010 karne kadhaa zijazo
 
You are gud man.
 
Kama binadam wa kwanza alitokana na sokwe, na sokwe wa kwanza alitokana na nini? haya mambo bana
 
Theory hazijitoshelezi. Lazima kuna nguvu iliyo na ufahamu nyuma ya uwepo wa maisha na ulimwengu. Vitu vipo systematic sana kusema vilitokea tu. Yaani mtu wa zamani huko anasema sokwe alibadilika akawa binadam na sisi tunaendelea kukariri. Haya sokwe alibadilika, na kitimoto je? Chenyewe kilikuwa nani hadi kikawa kina mafuta vile?
 
"Alionekana kijana mtu mzima kiasi kile..."wapi ulimuona ... Yani unaongea kama ulimuona?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…