Mwanzo wa kufeli kiuchumi Serikali ya awamu ya sita

Mwanzo wa kufeli kiuchumi Serikali ya awamu ya sita

Baba jayaron

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
4,324
Reaction score
5,933
Salam kwa Jamhuri

Kama raia wa kawaida mwenye mamlaka kamili kulinda na kuisimamia nchi yangu sitasita kuusema ukweli ninaoushuhudia na kuuchakata kichwani mwangu kisha kushauri inapobidi kutenda.

Dhahiri shahiri Serikali hii ya awamu ya sita haikujiandaa kwa lolote kuwepo madarakani, hivyo si ajabu kukosa muelekeo sahihi kuichumi kwa sababu:
1. Mitazamo ya awamu ya 5 na 6 ni tofauti na ilipaswa kuendeleza.
2. Inawezekana awamu ya 5 ilikuwa na friction nyingi kuliko uhalisia.
3. Hata sasa kuna mgongano wa ki ideology kwenye kuendesha Serikali.

Wakati awamu hii inashika hatamu ilijikita katika kufungua nchi pamoja kuomba mikopo na misaada na lakushangaza ilifanikiwa kupata mkopo mkubwa kuliko kutokea Jamhuri ya Tanzania.

Serikali imeshindwa kuelewa tatizo la nchi yetu si kupata mikopo misaada ama makusanyo bali ni usimamizi wake. Mega project hazieleweki hatma yake mpaka sasa.

Sasa impact ya hela zilizoingia bado hazionekani, mdororo wa uchumi unazidi kuongezeka ikiwa hakuna matumani.

Hakuna matumaini kwa sababu, mwazo tunalalamika na mifumuko ya bei inayosababisha ugumu wa maisha ilikaa kimya baadaye sababu ikawa haikujiandaa na vita ya Urusi na Ukrene (kisingizio) ambayo tulionja joto yake mapema wiki ya pili ya vita.

Juzi mama akafichua tulichofichwa kwamba hata uchumi wa kati tulishadodoka chaliii...

Sasa awali ya yote tulishaanzishia mitozo kedekede kabla sasa, je huko mbele Serikali hii imejipangaje kututumikia sisi wenye nchi tuliowapa dhamana kuboresha uchumi wetu?

Hii hali mbaya tunayoipitia isipo kuja na jawabu kabla hujawajibika wewe Mh. Rais unaebeba dhamana ya Watanzania wote tunakuomba uwajibishe Baraza la Mawaziri wako ama washauri wako wa uchumi.

Watu wamechoshwa na siasa za kuremba makaburi wakati ndani ni uozo, tunakutana uwajibike kweli kweli hii tabia ya kutengeneza sababu ya kila tatizo tumechoka tunataka suluhisho.

#kaziendelee!
 
Tozonia tozonia...nakupenda Kwa wallet yote.
Nchi yangu tozonia, Vizinga vyako vikubwa Sana..
Hatuwezi kusahau Sisi, mambo mema ya magu we...
Tozonia tozonia.. nakupenda Kwa kodi zote.
Wanatengeneza sumu watakayoshindwa kuitema
 
Kwa hali tunayopitia sasa hakukua na sababu ya kurudisha tozo ya sh 100 kwenye mafuta serikali ingebeba mzigo katika kipindi hiki cha mpito kwa kufanya yafuatayo
1. Kuzuia kwa muda semina, mafunzo warsha zisizo za lazima katika kipindi hiki. Kila nikiangalia taarifa ya habari unakuta zaidi ya 60% ya taarifa za kitaifa unakuta ni makongamano, kujengeana ujuzi nk na yanafanyika katika mahotel
2. Serikali ibane matumizi hasa kwenye safari za mawaziri na viongozi mbalimbali pamoja na watumishi
3. wasimamishe manunuzi ya vitu ambavyo kwa sasa sio lazima vinunuliwe kama magari nk

Itakapokuja kuisha vita ya Ukraine basi irudi kwenye biashara yake kama kawaida
 
Mtalizoea tu kama tozo za mitandao ya simu au bando kupanda bei ...baada ya wiki mbili tatu kutaibuka story nyingine na maisha yataendelea 🐒
 
Nadhani anatumia njia hii kurejesha pesa kenye mzunguko wa kawaida wakati ni njia yenye impact ndogo saana
 
Mtalizoea tu kama tozo za mitandao ya simu au bando kupanda bei ...baada ya wiki mbili tatu kutaibuka story nyingine na maisha yataendelea 🐒
Banana Republic sio?? Ila nna uhakika hali hii itawangusha mnoo hawatotoboa
 
Back
Top Bottom