SoC04 Mwarobaini wa ajira

Tanzania Tuitakayo competition threads

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
899
Reaction score
1,231
TANZANIA TUNAYOITAKA NA AFRIKA TUNAYOITAMANI NI ILE AMBAYO MFUMO WAKE WA MALEZI,UONGOZI NA ELIMU UNAWAJENGEA WANUFAIKA WAKE UWEZO WA KUJITEGEMEA BAADA YA MASOMO

Jukumu la kutengeneza kizazi chenye uwezo wa kujiajiri sio la mamlaka za elimu tu bali hata walezi.

Walezi wengi wanapeleka watoto wao kwenye taasisi za masomo wakiamini ndio chombo pekee kinachoweza kufungua maisha yao kumbe sio sahihi.

Miongoni mwa mambo ambayo naamini jamii,taasisi za elimu na serikali inapaswa kuyafanya ili kubadili mfumo huu ni kama ifuatavyo;

Mambo haya yatalenga kuondoa vikwazo kwenye mambo makubwa matatu yanayokwamisha vijana kujiajiri ambayo ni kukosa uwezo wa kazi za mikono,kukosa mitaji na kukosa uzoefu (experience)

A.Kukosa uwezo wa kazi za mikono (manual work).
Vijana wengi wanateseka mtaani sio kwa kukosa elimu bali ni kukosa ujuzi wa mikono.
Asilimia kubwa ya graduates wetu wana uwezo mkubwa wa kazi za akili (intellectual work) na sio kazi za mikono (manual work) jambo ambalo linawatesa linapokuja swala la kujiajiri.

Jukumu la familia-Wazazi wanapaswa kuwapeleka watoto wao kwenye karakana kulingana na utashi wa mtoto kila mwisho wa juma.Mtoto wa miaka 7-14 akipata nafasi ya kutumia masaa 48 katika week kushinda kwenye karakana ya samani,kutengeneza simu na kompyuta,kutengeneza .’software &applications’,ususi,ushonaji,upambaji nk kwa hakika mpaka kufikia miaka 14 atakuwa mbombezi.

Ujuzi atakaoupata utatengeneza mapenzi ya kusomea zaidi anachokijua kukifanya na muda mwingine inaweza kuwa ndio ajira yake kama hatofika mwisho wa mfumo wa elimu.

Jukumu la serikali na taasisi za elimu-Mambo mawili makuu yanayopaswa kufanywa kwanza ni
1.Mfumo wa elimu unapaswa uweke nguvu nyingi kwenye elimu ya vitendo zaidi.

2.Somo la ujasiriamali linapaswa kufundishwa darasani na kwa vitendo kuanzia ngazi ya msingi mpaka elimu ya juu.

3.Lazima ijengwe miundombinu itakayokuwa na karakana mbalimbali mashuleni ambazo tutatumia walimu wa VETA kuwafundisha watoto kazi za mikono.

4.Serikali inapaswa kufufua na kuongeza ‘techinical schools’ kila wilaya Tanzania.

5.Taasisi za SIDO na VETA zinapaswa kuunganishwa na kutumiwa na taasisi zote za elimu kuanzia ngazi ya awali mpaka chuo kikuu kufundisha kazi za mikono na ujasiriamali.

Naamini kama 80% ya watahiniwa wetu wakiwa na ujuzi wa mikono na elimu ya ujasiriamali basi tatizo la ajira tutalipunguza kwa asilimia 50%.

B.Ukosefu wa mitaji.
Swala la ukosefu wa mitaji kwa kiasi kikubwa limekuwa likitupiwa lawama serikali kama ni swala la ghafla lakini kwa kiasi kikubwa lilipaswa kutatuliwa na ngazi ya familia.

Jukumu la familia-Jamii zetu za kitanzania na Afrika hatuna utamaduni wa kuwekeza (kufanya saving) kwajili ya maisha ya watoto wetu baadae.Wazazi wamejivika jukumu la kusomesha tu ajira wameiachia serikali.

Wazazi na walezi wanapaswa kuwekeza kiasi kidogo cha pesa au mali zao kuanzia mtoto amezaliwa mpaka atakapomaliza masomo yake ya juu,pesa hii ni ukombozi mkubwa sana mtoto akikabidhiwa kama mtaji pindi tu atakapomaliza masomo yake.

Uwekezaji pia unaweza kuwa kwa njia ya mali kama mashamba ya miti,viwanja,hisa kwenye makampuni mbalimbali,hati fungani (ie UTT) nk.

Tukiwajengea utamaduni huu watoto wetu itakuwa rahisi na wao kuwekeza kiasi kidogo cha pesa za kujikimu wanazopata kupitia kazi zao za mikono na mikopo ya elimu ya juu kwa njia zile zile wazazi wao walizotumia kuwawekezea.

Jukumu la serikali na taasisi za elimu;Ni dhahiri shahiri kwamba mfumo wa mikopo ya vikundi kupitia halmashauri ni mfumo uliofeli hivyo basi nashauri mambo haya yafanyike;

1.Wahitimu wa vyuo vya juu na vya kati wanapaswa wapewe posho ya ujasiriamali (entrepreneurship allowance) pesa ambayo inakwenda kuwa ni mtaji wa kwanza kwenye maisha yao ya utafutaji.

Binafsi siamini kama umeweza kumuamini kijana kwa kumkopesha mkopo kwa miaka mitatu ushindwe kumkopesha mtaji wa kuanzia maisha.Pesa hii inapaswa kutolewa kupitia bodi ya mkopo miezi 6-12 baada ya wahitimu kumaliza masomo yao.

C.Kukosa uwezo wa kujitegemea na uzoefu.
Jukumu la walezi-Familia zinapaswa kubadili mfumo wao wa malezi kwa kuwaingizwa watoto wao moja kwa moja kwenye mfumo wa kitu kinachoingizia familia kipato.Tunapaswa kujifunza kwa wenzetu wa jamii ya Asia ambapo mtoto hutumia siku za mapumziko na likizo zote kushinda kwenye biashara ya familia akijifunza.

Kama mzazi ni mkulima basi watoto wanapaswa wafundishwe kilimo,kama mzazi ni seremala basi watoto wanapaswa kufundishwa useremala.

Jukumu la serikali na taasisi za elimu-Muda wa masomo kwa vitendo (field work) unapaswa kuwa asilimia 50% ya masomo ya mwanafunzi wa ngazi yeyote ya elimu hasa chuo kikuu.
Serikali ina nafasi 2 ya kujengea wahitimu ujuzi na uzoefu;

1.Kuongeza wigo wa kada ambazo wahitimu wake watapewa nafasi za mafunzo ya utayari (internship) mbali na kada za afya.

2.Kuandaa semina mbalimbali kwa kushirikiana na VETA,SIDO na makampuni makubwa ili kuwajengengea ujuzi wa ziada watahiniwa hao.

Binafsi kama walezi na nchi kwa ujumla tutayafanya haya basi tutaipata tanzania yenye ajira tunayoitaka na Afrika yenye maendeleo tunayoitamani.
 
Upvote 3
Nashukuru kwa mchango wako mzuri; shida ninayoiona tukitaka kutekeleza hilo ni jinsi ya kuwabadilisha watu mawazo (mindset) ndiyo kikwazo cha kwanza hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…