Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 441
- 1,065
Katika huduma ambayo inazidi kuwa ghali na inachukua maisha ya watu wengi ni ukosefu wa huduma bora za afya
Wakati mwingine watu hupoteza maisha si kwa kutokuwepo kwa madawa au wataalamu wa afya wenye uwezo bali ni kwasababu ya kukosa pesa za kugharamia matibabu na kutoa hongo kwa wahudumu
Kuna kisa kimoja kiliwahi kunikuta kwenye hospitali kubwa kabisa ya serikali mwaka 2012 mgonjwa wetu ilibaki kidogo tumpoteze kwa kuchelewa kupata maelekezo sahihi ya nini daktari anachotaka (kuzungushwa sana maana wala rushwa hawanyooki). Bila nesi mmoja kutuonea huruma na kutukonyeza pembeni tujichange tumpe daktari kiasi cha Tsh.300,000/= tungempoteza
Ifahamike kuwa ni jambo gumu sana kubadili mind set za wahudumu wengi wa afya kuhusu hizi hongo ndogo ndogo wanazotegemea kutoka kwa wagonjwa
Ili kulifanikisha hili, viongozi waandamizi katika sekta hii ya afya inawapasa kulivalia njuga swala hili na walifanye kwa mfumo wa kutoa elimu kuliko vitisho ambavyo mara nyingi havisaidii
Sasa hivi karibu kila hospitali kubwa wamefunga kamera za ulinzi ikiwa na lengo mojawapo la kubaini wahudumu wanaopokea hizo hongo. Lakini hili halisaidii sana badala yake limeleta tatizo lingine la wahudumu kutowajibika
Kukiwa na elimu za mara kwa mara kwa hawa wahudumu wa afya angalau litawajengea ari ya kuwajibika na aibu ya kudai rushwa kwa wagonjwa
Hili linawezekana kwasababu nimeona kwenye baadhi ya halimashauri ambapo walimu walikuwa wananyanyaswa na viongozi wao hadi wahudumu wa ofisi kwa kupitia vikao mbalimbali vya kuelimishana na kusemana siku hizi changamoto hiyo imepungua kwa asilimia kubwa na walimu wa halimashauri hiyo wanahudumiwa vizuri na wanafurahia uwepo wao kazini.
Kama hili limewezekana katika idara ya elimu, naamini kabisa na kwenye afya linawezekana kwani binadamu wameumbwa na haya. Wahudumu wetu wakielezwa kwa mifano watu wanaopoteza maisha kwa kukosa huduma nzuri kisa wameshindwa kutoa hongo, na wakaelezwa namna damu za hao watu zinavyowalilia huko toharani na pengine kuwaletea mauza uza kwenye maisha yao wengi watabadilika
Swala la msingi hapa sio kwamba hawayafahamu hayo, swala kubwa ni kwamba hawasemwi na kusimangwa ili wajione wana hatia. Ujue unaweza kufanya dhambi hala usipo pata mtu sahihi wa kukusema huwezi kuona hatia ya ulichofanya ila akipatikana wa kukueleza kwa usahihi madhara ya unachofanya hakika binadamu tumeumbwa na haya na lazima wengi watabadilika
Hili linatakiwa kwenda sambamba pamoja na kuwajenga wataalamu wa afya wakiwa bado kwenye mafunzo huko vyuoni kuelewa mikosi wanayojiwekea kwa kusababisha vifo kisa hongo ambazo haziwafikishi popote.
Jambo lingine ni kuondoa mianya ya kupokea keshi kwenye vituo vya afya. Hili linawezekana kwa kuwezesha bima ya afya kwa wote
Tukirudi kwenye sekta ya elimu kidogo, baada ya kufuta ada mashuleni kuna namna wazazi wamepata ahueni ya kudaiwa michango mingi isiyokuwa rasmi kama ilivyokuwa wakati walimu wanapokea fedha kutoka kwa wazazi
Kwenye vituo vya afya tukifikia hatua ya mgonjwa kwenda na kadi tu kwa ajili ya matibabu wahudumu wetu watawajibika tu kwasababu kutakuwa na ufanano wa wagonjwa. Hakutakuwa na mgonjwa anayepewa kipaumbele kama ilivyo sasa kwa wenye pesa kupewa kipaumbele
Hatua hii ni ya juu sana lakini inawezekana kama serikali ikiamua.
Kwa kuanzia tunaweza kupendekeza sheria itungwe ambapo kila mtoto anayezaliwa mama asiruhusiwe kutoka hospitali hadi amekata bima ya Mama na mtoto angalau ya miaka mitatu. Hili linawezekana kwasababu Mama mjamzito ataanza kupewa elimu na kujengwa kisaikolojia toka akiwa mjamzito anapohudhuria kliniki. Hii itasaidia kufanya maandalizi ya pesa pia. Hapa serikali iache bla bla zake za kwamba watoto chini ya miaka mitano wanatibiwa bure kwasababu hakuna kitu kama hicho kiuhalisia
Jambo lingine ni kwa wanafunzi. Iwe ni sheria kuwa kila mtoto anayeandikishwa darasa la kwanza anakatiwa bima ya afya na linakuwa ni takwa la kisheria la kulipia bima hiyo kila mwaka. Hili ni rahisi sana kwasababu serikali imefuta ada mashuleni kwa hiyo Bima inaweza kuchangiwa kwa stili hiyo ya kama kulipia ada
Utamaduni huu ukijengwa kwa watoto wataambukizwa hadi watakapokuwa watu wazima wataona ni jambo la kawaida na hawatalazimishwa tena. Hili sio gumu kwasababu NHIF walipoanzisha bima ya afya kwa wanafunzi halafu baadae wakaiondoa kwa sababu zao wenyewe unaweza kuona namna wazazi wengi wanavyotamani irudishwe
Binafsi huwa najiuliza, benki hazitoi mkopo bila mkopaji kukatwa bima ya mkopo, vyombo vya moto hususani magari yanakamatwa na askari wa usalama barabarani wanapokuwa hawajakata bima za magari yao. Lakini kwa maisha ya watu hawaoni umuhimu huo?
NHIF wakati inaanza kukata makato ya Bima kwa wafanyakazi, wafanyakazi wengi walikuwa hawapendi na walilalamika sana. Lakini leo kamuulize kama kuna mtumishi wa umma bado haoni umuhimu wa bima ya afya. Wengi sana NHIF imekuwa mkombozi kwao na hata ukitembelea vituo vya afya vya serikali na binafsi vile vinavyopokea NHIF ndivyo vinaongoza kwa kutoa huduma nzuri ambayo ni tafsri ya faida wanayopata na wafanyakazi wanapata ahueni ya matibabu.
Bima ya afya itasaidia sana kuondoa rushwa kwenye vituo vya afya kwasababu watu watabeba kadi badala ya pesa na kwasababu hiyo uwajibikaji utaongozeka
Kitu kingine ni kusimamia sheria zinazohusu haya maguka ya madawa. sheria inawataka kumuuzia dawa mgonjwa mwenye karatasi ya maelezo ya daktari. Lakini hili halisimamiwi na hakuna sababu inayofanya lishindikane isipokuwa uzembe tu wa watendaji wa serikali.
Hili la kutosimamia famasi kuuza madawa holela linachekesha kama ilivyo sheria ya kutowauzia pombe watoto chini ya miaka 18 halafu kila wekeend wanajazana kwenye kumbi za starehe na hawafukuzwi. Huu ni mzaha!
Serikali ikiacha siasa katika maswala ya msingi kama Bima ya afya, watu wote wanaweza kulipia bima ya afya na sera ya bima ya afya kwa wote ikawa halisi kuliko ilivyo sasa.
Pia soma: