Monasha
JF-Expert Member
- Apr 2, 2011
- 561
- 422
MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila, amewatoa hofu wagonjwa wa Ukimwi ambao wamepata tiba yake na baada ya kupimwa wameendelee kukutwa na virusi vya ugonjwa huo.
Akizungumza kabla ya kuanza kutoa tiba jana nyumbani kwake Samunge, Mchungaji Mwasapila alisema mgonjwa wa Ukimwi mara baada ya kupata kikombe, virusi vya HIV vitaendelea kupukutika taratibu na havitazaliana tena.
"Napenda kuwaondoa hofu wenye Ukimwi kwamba ukitumia kikombe, utaona mabadiliko ya afya yako baada ya siku saba tu, lakini unaweza kupima na kujikuta bado unavirusi, usiwe na hofu vitapukutika na mwisho vitakwisha vyote mwilini," alisema Mwasapila.
Mwasapila alisema mabadiliko ya afya kwa wenye virusi vya Ukimwi yatakuwa kati ya siku saba na 21 na kama mgonjwa na anahofu, anaweza kuendelea kutumia dawa zake za kupunguza makali ya ugonjwa huo (ARVs), ila alisisitiza kuwa dawa yake inatosha kuponya.
Je wewe mwanajamiii unasemaje kwa hili la Babu. Ataweza kuponya UKIWMI au ni porojo tu??
Naomba pia kama una mtu uliyemwona kapona kabisa basi usisite kutueleza ukweli wanajamii wenzako.
Mi si mwamini babu.