Mwasheria Mkuu ajiuzulu kwa lipi?

Mwasheria Mkuu ajiuzulu kwa lipi?

Rege

Senior Member
Joined
Jul 9, 2022
Posts
117
Reaction score
153
Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaandamwa eti ajiuzulu kwa kashfa ya nchi kusaini mkataba wa Bandari na Dubai, yeye kosa lake ni lipi ikiwa hakuna saini yake kwenye mkataba huo?

Kwanini mnamuacha aliyehusika kusaini mkataba mnataka kumuangushia jumba bovu Jaji Feleshi?
 
Ibara ya 59 (3) ya katiba ya 1977 inasema

Mwanasheria Mkuu atakuwa ndiye mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na, kwa ajili hiyo, atawajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria zitakazopelekwa kwake au atakazoagizwa na Rais kuzitekeleza,
na pia kutekeleza kazi au shughuli nyinginezo zilizokabidhiwa kwake na Katiba hii au na sheria yoyote
.

Kuwajibika kwake kunaanzia hapa
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, anaandamwa eti ajiuzulu kwa kashfa ya nchi kusaini mkataba wa Bandari na Dubai, yeye kosa lake ni lipi ikiwa hakuna saini yake kwenye mkataba huo.

Kwanini mnamuacha aliyehusika kusaini mkataba mnataka kumuangushia jumba bovu Jaji Feleshi?
Kwa mujibu wa sheria aliyesaini ndio anatakiwa kusaini?
Kwa mujibu wa sheria je ambaye hakusaini ndio anatakiwa kusaini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu mkataba ulosainiwa una mapungufu mengi, ajisimama MZALENDO mmoja tu, tunawafurusha DP world.
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, anaandamwa eti ajiuzulu kwa kashfa ya nchi kusaini mkataba wa Bandari na Dubai, yeye kosa lake ni lipi ikiwa hakuna saini yake kwenye mkataba huo.

Kwanini mnamuacha aliyehusika kusaini mkataba mnataka kumuangushia jumba bovu Jaji Feleshi?
Siasa tu .....

Siasa kinzani tu....

Siasa za chuki tu.....

Mh.Rais SSH tuna imani kubwa na serikali yako [emoji123]

#SiempreJMT[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Fatuma ndo atakuwa kaanzisha hili,kisa tu enzi za Magufuli .Feleshi alipokuwa jaji kiongozi alimtemesha Fatu uwakili.
 
Fatuma ndo atakuwa kaanzisha hili,kisa tu enzi za Magufuli .Feleshi alipokuwa jaji kiongozi alimtemesha Fatu uwakili.
Baba mdogo Mzee Ali anashambulia kutokea Zanzibar....

Mtoto wakili anafyatua mabomu kutokea Bara.....

Chuki tu dhidi ya utawala wa mh.Rais SSH.....[emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Watakuwa walimruka AG au walipuuza ushauri wake wa kisheria (hawalazimiki kufuata ushari BTW, ile sio hukumu ya mahakama). Hata viongozi wengine waandamizi serikalini wako kimyaa, ndio ujue huu ulikuwa mchezo wa wachache.

Yaani kama namuona Mbarawa akimwambia katibu mkuu wa wizara "saini hapaa"
 
Huu mkataba ulosainiwa una mapungufu mengi, ajisimama MZALENDO mmoja tu, tunawafurusha DP world.

Too late, adui unae ndani kila mahali, nchi ilishaenda hii, sasa jitayarisheni kupanda rwanair badala ya Air Tanzania yetu, jiulize nani aliyepeleka Ndege yetu Uholanzi ili ikamatwe?
 
Too late, adui unae ndani kila mahali, nchi ilishaenda hii, sasa jitayarisheni kupanda rwanair badala ya Air Tanzania yetu, jiulize nani aliyepeleka Ndege yetu Uholanzi ili ikamatwe?
Mungu atajitwalia Utukufu.

Tumepambana vya kutosha, tumetimiza wajibu wetu kusema na kupinga lakini tunapuuzwa.

Tusubiri.
 
Back
Top Bottom