TANZIA Mwasisi wa CHADEMA, Edwin Mtei afariki Dunia

Huo ubepari alioutaka unaihangaisha dunia nzima hivi sasa, maandamano kila kukicha huko USA maana yake sera hizo pia zinafeli tena kwa kasi.
Hapa Tanzania haifanyi ubebari kwa sasa? Au haujui maana ya ubebari? Tatizo hapa ni wanafiki hamtaki kukiri nyie ni mabepari ndiyo maana Mtei alikataa unafiki wenu akajitenga na nyie wanafiki. Na alikuwa sahihi. Mlichokataa 1979 ndicho mlikuja kuimplement kwenye utawala wa Mwinyi.

Hata kuondoka Nyerere madarakani ni baada ya kuona sera zake za kinafiki zimefeli akaona aibu kula matapishi yake
 
Nyerere alishachoka pia alihisi dunia itambadilikia mbele ya safari.
 
Pumzika Mzee Mtei.

Pole kwa familia.

Kama mpenda vitabu nimefurahia sana kusoma kitabu cha maisha yake "From Goatherd to Governor : The Autobiography of Edwin Mtei".

Kitabu kina historia kubwa sana sio tu ya Mtei, bali pia ya Tanzania.
 
Mtei kama Polepole vile.
Ukiona hukubaliani na namna nchi inavyo endeshwa unajitoa kwenye huo uongozi.
Ila Polepole alisema bado ni mwanaccm mtiifu na ndiyo hapo alipozingua au muda haukumtosha kufanya maamuzi tofauti. Hata Warioba nilishangaa hivi karibuni aliposema yeye bado ni mwanaccm mtiifu.
 
Hapa kwenye kutumia pesa zake na rasilimali zake.
 
RIP Mzee,
Kaondoka na Chama Chake Kuwa Cha Upinzani Mbinguni.
Wasalimie Mwalimu JK,na Mrema huko.
 
May his soul rest in eternal peace!

Tumetoka mbali. Zama hizi bila kuwa distinguished economist, sio rahisi sana kuteuliwa kuwa governor wa benki kuu!
 
Pumzika kwa amani Mzee Mtei
Mtei ali 'set the bar' katika utumishi wa Umma. Kwamba alimkatalia Nyerere sera za kifedha na kujiuzulu.
Mwl Nyerere alikubaliana naye, wote wakaishi nchi moja bila kutekana, kuviziana au kutungiana kesi za uhaini. Kwamba walikubaliana kutokukubaliana bila visasi chuki au indhara.

Mtei alikataa UCHAWA! wakati watu wanaandamana kupinga sera za IMF kishabiki, mtei aliwapinga hadharani.
Leo hii tunaishi na sera zile zile alizozisimamia Mzee Mtei ingawa zilikataliwa

Mzee Mtei na Bob Makani (RIP) walianzisha CHADEMA Nyerere akiwa hai! hawakupewa kesi za uhaini!! Hawakupokea simu za vitisho au Familia zao kuhujumiwa. Tuliishi Nchi moja ya Tanzania kwa Amani.

Tuliishi kwa AMANI kwasababu wao walitenda HAKI na walitendewa HAKI.

Mazishi ya Mzee Mtei yanapaswa kuchukua sura ya Kitaifa!

JokaKuu Mzee Mwanakijiji
 
Leo mpaka anakufa kwa sonona kwa jinsi milugaluga na miporipori iliyovamia siasa ilivyokiharibu chama
 
Mtei alikataa ujinga wa sera za ujamaa zilizofilisi nchi huku viongozi wakineemeka na ndiyo sababu ya yeye kupingana na Nyerere na hatimaye kuondoka Serikalini
Huo ujamaa wa kuwatajirisha viongozi ni upi? Ingekuwa ni ubepari si ungekuta familia ya Nyerere ndio wanamiliki njia nyingi za uchumi hapa Bongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…