Mwasiti aanika maisha yake ikiwemo mara yake ya kwanza kuvunja amri ya sita

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
katika gemu la muziki wa Bongo Fleva, Mwasiti Almas amefunguka ‘exclusive’ kuhusiana na maisha yake kwa jumla ambapo kwenye masuala ya uhusiano amebainisha kuwa alimjua mwanaume mara baada ya kumaliza kidato cha nne.
Alisema alijitunza sana akiwa shule ya msingi, akaendelea hivyo hadi alipomaliza masomo ya sekondari ndipo alipolegeza uzi na kujikuta ameanza kuvunja amri ya sita na kujua thamani ya mwanaume.
“Nilikuwa muoga sana, tangu shule ya msingi hadi sekondari sikuweza kabisa kufanya mambo ya kikubwa,” alisema.
Akizungumza na Weekly Star Exclusive, Mwasiti alifungukia umri wake ambapo alikiri ‘eji’ imeenda lakini suala la kuolewa ataendelea kusubiri hadi muda muafaka utakapofika.
“Kuhusu umri kwa sasa nipo katikati ya 25 hadi 30, umri umeenda kidogo siyo mdogo mimi. Nitaolewa tu muda ukifika, sina haja ya kuharakisha,” alisema Mwasiti.
Japo hakuanisha muda muafaka wa kuolewa, katika sentensi nyingine Mwasiti alisema anatamani sana kuzaa mwaka huu kwani amekuwa na hamu ya kuitwa mama.
Mwasiti ambaye juzikati ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Serebuka (audio na video), hivi karibuni alivuta mkoko mpya aina ya Rav 4 huku akiwa mbioni kukamilisha mjengo wake maeneo ya Mbezi ya Kimara, jijini Dar.
 
mbona hajanitaja niliemfungua daaa masem bhana
 
Hivi uzinzi siku hizi unashabikiwa hadharani? Vipi padri au sheikh wake akisikia ujinga huu?
 
Yaani kufanya mapenzi baada ya form four ndio anaona amejitunza!! heri angebaki na hiyo siri moyoni maana kuitamka hadharani sidhani kama ni sahihi , naamini kuna wasichana wadogo Mwasiti ni role model wao, hivyo nao wakimaliza form four tu wataona huo ndio muda muafaka wa ngono.
 
Ulikua ujui? Hao ndio mastar wetu ila bora amesema ukweli

Hafadhari mara 100 ya Lulu aliyekuwa kwenye interview anasema yeye ni bikra anakuwa amewasaidia watoto wengi ila wazee wamujini tunajuwa kinachoendelea.

Siku si nyingi wataanza kujinasibu walifanya mapenzi kinyume na maumbile mara moja tu.
 
Hafadhari mara 100 ya Lulu aliyekuwa kwenye interview anasema yeye ni bikra anakuwa amewasaidia watoto wengi ila wazee wamujini tunajuwa kinachoendelea.

Siku si nyingi wataanza kujinasibu walifanya mapenzi kinyume na maumbile mara moja tu.

ilo la kujinasibu kufanya mapenzi kinyume cha maumbile mbona tayari nilileta thread ya lulu akijinasibu kufanya kinyume nakutafutia sasa hivi subiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…