Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 384
- 970
Mwathirika na Mhanga. Mwathirika ni ama mtu anayepatwa na jambo linalomsababishia madhara bila ya yeye kukusudia au mtu anayefuata tabia na mienendo ya mtu mwingine. Hivyo, dhana hii inaweza kuwa na maana chanya au hasi. Wako watu walioathiriwa na mienendo na tabia nzuri za walimu wao, wazazi wao, walezi wao, marafiki wao na hata majirani wao. Hata hivyo, wako pia walioathiriwa vibaya kama vile na mafuriko, vita, uvamizi, ukame, tetemeko, magonjwa n.k. Katika matumizi mtu anaweza kusema, ‘Mwathirika yule wa mafuriko amepatiwa hema’ au ‘Juma ni Mwathirika wa tabia na mwenendo wa mwalimu Nehemia.’ Hapa tunakusudia kuondoa dhana mbaya iliyojengeka katika jamii yetu ya kuhusisha kuathirika na ugonjwa wa UKIMWI.
Mhanga kwa upande wake, tukiacha maana ya mnyama anayesifika kwa kuchimba na kuishi kwenye mashimo, ni mtu anayeyatoa maisha yake kwa ajili ya maslahi yake, kikundi, jamii au taifa lake. Mhanga hufanya hivyo kwa kudhamiria, na hii ndiyo tofauti kubwa kati yake na Mwathirika ambaye aghalabu hukumbwa na baa bila ya kutarajia. Katika matumizi inaweza kuwa: ‘Wahanga wawili wamepoteza maisha yao na ya wengine kadhaa baada ya kujilipua sokoni.’ Mfano mwingine unaweza kuwa, ‘Mhanga mmoja alikamatwa uwanja wa ndege akiwa amejifunga mabomu.’