MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 716
- 1,143
Nakua kama naota vile, sijui ni kweli au naota mchana jamani, eti Pandu Kificho mwenyekiti wa muda wa bunge maalum ameinda kamati ya kuchunguza kama malipo ya laki tatu 300,000 wanazolipwa wajumbe wa bunge la katiba ichunguzwe kama inafaa au iongezwe. Jamani mbona tunafanyia hivyo, mimi nimwalimu kwa taaluma na nimeajiriwa halmashauri ya Bagamoyo nalipwa 470000 kwa mwezi pamoja kuwa na shahasa ya chuo kikuu, tena naidai serikali mishahara yangu miwili kwa sababu wakati naanza kazi sikulipwa miezi 2 na toka mwaka 2011 nimekua nazisotea hizo pesa bila mafanikio, siyo mimi peke yangu, kwenye kituo napofanyia kazi walimu wote 14 tunaidai serikali malimbikizo hayo ya mishahara na wengine fedha ya uhamisho.Chama cha walimu wakiitisha mgomo ili serikali itupe hela yetu mawakili wa serilaki wanakwenda kuweka pingamizi tena usiku wakati majaji wamelala eti kubatisha mgomo lakini sioni hata mara moja bunge likiunda kamati ndogo kama hiyo kuangalia madai hayo, halafu mnategemea Big Results Now kutoka kwa walimu walionyimwa stahiki zao. Kumbukeni kwamba walimu wengi wanaishi kwa mikopo na wengine hupokea hata chini ya laki moja kwani wamekopa kwenye mabenki zaidi ya moja. Halafu wajumbe mnasema posho ya laki tatu kwa siku haiwatoshi jamani, huo ndio uzalendo na wito mnaoutaka walimu na waganga waunyeshe kwa jamii ilihali nyie hamna hata chembe ya uzalendo kiasi hicho? Jamani eti hamuwezi kulala kwenye guest za uchochoroni, wenzenu huku pamoja na madgree tuliyonayo tunalala kwenye nyumba za majani, hakuna maji, umeme, barabara, zahanati, mtandao, barabara wala huduma yoyote ya jamii unayoijua wewe lakini mbona tunaishi, tena ni kwenye jimbo la mheshimiwa rais. Kama kweli kamati ikija na pendekezo la kuongeza hiyo posho nitaacha kazi na niwe mkulima tu ili nisiendelee kuitesa nafsi yangu kwa manunguniko maana najua hata kama nikisema niendelee na kazi ufanisi utakua zero kwani muda wote nitakua nawaza unyonge wa kazi ya ualimu. Bora nifanye kazi nyingine kuliko chukizo hili la ajabu kwa wachache kula nchi huku mimi nikiidai serikali bila dalili zozote za kulipwa.