KERO MWAUWASA jitafakarini na chukueni hatua stahiki za haraka! Maji sio Anasa, ni takwa la mahitaji muhimu ya binadamu!

KERO MWAUWASA jitafakarini na chukueni hatua stahiki za haraka! Maji sio Anasa, ni takwa la mahitaji muhimu ya binadamu!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

makachu Makachu

New Member
Joined
Jan 13, 2025
Posts
4
Reaction score
4
Watendaji idara ya maji Mkoa wa Mwanza Jitafakarini na chukueni hatua za haraka!Eneo Na mitaa ya Nyegezi stendi.

Mwanza ni jiji kubwa ambalo, kwa idadi ya watu, ni jiji la pili kwa Tanzania.

Kumekuwa na changamoto kubwa sana ya maji ambayo haieleweki, na watendaji wako wametulia kabisa bila kutoa majibu.

Kwa makadirio, baadhi ya maeneo ya mijini yanapata maji kwa takriban mara Moja kwa nayo yakitoka nikama tone ndani ya wiki mbili, na sehemu fulani hakuna maji kwenye mitaa; mfano, katika Nyegezi, stendi ambapo ni mijini hakuna maji kabisa katika mitaa mingi.

Serikali imekamilisha mradi wa maji butimba, lakini kumekua hadithi tu; maji hayupo, wala taarifa sahihi hazipo.

Enyi watendaji, tuambieni: mnalipwa kodi za nani?

Madharani Kila mwezi , bili za maji kila mwezi mnatuma Tena kubwa mnazotoa wapi?

Tunaomba viongozi wa idara ya maji, ngazi ya juu: tokeni ofisini, piteni mitaani, na ulizeni kwa raia hawa vijana michezo; hakuna maji!

Waziri husika, tunaomba ufanye ziara; tembelea mitaa. Usiende tu kwenye mitaa uliyo pangiwa, bali piga hatua kuelekea mitaa ambayo hawajakupangia. Utapata ukweli wa tatizo hili la maji.

Katika mitaa mingine, maji yanatoka kama tone la "Moja la Mvua". Kuna shida gani? Au mnasubiri ziara za viongozi wakubwa, mnafungulia maji mpaka mabomba yanapasuka?

Mfano, katika kila mtaa, katika kilele cha mwenge au ziara ya Mweshimiwa Raisi maji yanatoka Hadi mabomba yanapasuka watu wanauliza yanatokea wapi?

Tambueni , mnaishi kwa kodi zetu! Msisubiri uchaguzi, hapo ndipo mnatoka kutudanya katika mitaani.

Chukuni hatua ya haraka kusuluhisha jambo hili.

Cc: Waziri wa Maji & Mkuu wa Mkoa wa Mwanza

Pia soma > KERO - Idara ya Maji Nyegezi Mwanza (MWAUWASA) jitafakarini suala la ukosefu wa maji
 
MWAUWASA Vision:
To excel and become a leading water and sanitation utility in Africa.

MWAUWASA Mission:
To provide adequate potable water and sanitation services in Mwanza City at optimal cost.
 
Inasikitisha sana maji yamekua tatizo kubwa wakati ziwa lipo karibu
 
Back
Top Bottom