KERO MWAUWASA tunataka maji mtaa wa Mwananchi mkoani Mwanza

KERO MWAUWASA tunataka maji mtaa wa Mwananchi mkoani Mwanza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Sasa yapata wiki Mtaa wa Mwananchi hatupati maji hatuelewi kuna tatizo gani. Mhe. Waziri wa Maji fanya mabadiliko ya haraka katika Mamlaka ya Maji Jijini Mwanza(MWAUWASA) ili wananchi tuwe tunapata maji ya uhakika.
 
Kuna mchina kapewa kiwanja pale Mwanza food juu ya bomba kuu linalopeleka maji Mwananchi hadi Mahina. Kajenga juu yake na kuliondoa hilo bomba. Hiyo sehemu ni open space na ni swampy area kwenye ramani inajulikana kwa jina la Arab Land.
 
Pole mkuu najua pain yako, yaani jamaa kuhamisha bomba mita 50 wanatumia wiki kadhaa .Haya maajabu
 
Sasa yapata wiki Mtaa wa Mwananchi hatupati maji hatuelewi kuna tatizo gani. Mhe. Waziri wa Maji fanya mabadiliko ya haraka katika Mamlaka ya Maji Jijini Mwanza(MWAUWASA) ili wananchi tuwe tunapata maji ya uhakika.
Nilipita hapo juzi naona wanafungafunga,ivi walitoa taarifa ?
 
Mwauwasa ni moja ya taasisi mbovu iliyochini ya serikali kwa mfano hapa Buhongwa, Buguku, Sahwa ya juu na chini mitaa yote hii hakuna maji kabsa na wananchi wanapata shida kutafuta maji kwenye mabonde ya mito ili hali ziwa victoria lipo ndani ya KM8.
 
Uko mwananchi wiki tu mnalia malimbe kuna eneo hamna maji miezi miwili+ na hata hawashtuki hao Mwauwasa na kila mwezi bili lazma ije 5k+
 
Mwauwasa ni moja ya taasisi mbovu iliyochini ya serikali kwa mfano hapa Buhongwa, Buguku, Sahwa ya juu na chini mitaa yote hii hakuna maji kabsa na wananchi wanapata shida kutafuta maji kwenye mabonde ya mito ili hali ziwa victoria lipo ndani ya KM8.

Ile tanki kubwa la maji hapo sahwa halijaisha tu?
Lilikua linajengwa na wachina?
 
Back
Top Bottom