Mwe!

eRRy

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Posts
1,126
Reaction score
206

MAJED ELMALK, raia wa Saudi Arabia, ambaye hivi sasa anashikilia rekodi ya dunia ya kuweka mdomoni nge wengi zaidi, anaonekana akipigwa picha mjini Riyadh siku ya tarehe 22 Januari mwaka huu akiwa na nge kibao mdomoni na baadhi yao wakiwa wametoka nje.
Mtu huyo, kama anavyoonekana pichani, hana wasiwasi wowote na wadudu hao wakali na wenye sumu na ambao huogopewa sana na watu. Elmalk anaweza kusokomeza mdomoni makumi kadhaa ya wadudu hao mdomoni mwake
.



MSICHANA mmoja nchini India amekuwa kivutio kitakatifu ambapo watu wa dini yake huenda kumtazama anapolia, kwani huwa anatoa machozi ya damu.
Madaktari huko Patna, kaskazini-mashariki mwa India, wameshangazwa na hali ya msichana huyo aitwaye Rashida Khatoon, wakishindwa kujua ni nini humfanya atoe machozi ya damu mara kadhaa kwa siku moja.
Hata hivyo, viongozi watakatifu wa madhehebu ya Kihindu, wamemtangaza msichana huyo kuwa ni muujiza wa dini yao.
Hivi sasa wafuasi wa madhehebu hayo hujazana nyumbani kwa msichana huyo wakimpa zawadi mbalimbali kama matoleo ya utakatifu.
Alipohojiwa kuhusu hali hiyo, Rashida alisema: "Huwa sisikii maumivu yoyote inapotokea hivyo, lakini ni jambo la kushitua kuona damu inatoka badala ya maji."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…