MtuMzima News
New Member
- Feb 27, 2024
- 1
- 0
Kitendo cha Mwekezaji kupelekewa maji na Wananchi kukosa, kimeibua maswali kwa Wananchi wa Kitongoji cha Mgodini, Nyakavangala, Kata ya Malenga Makali, Wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
Mwekezaji huyo amepelekewa maji, huku Wananchi wenye uwezo mdogo wakinunua maji kwa ndoo moja TZS 500/-, huku wasio na uwezo wakilazimika kutumia maji ya kwenye madimbwi.
Wananchi hao zaidi ya 1,000, wamekuwa wakitaabika kupata maji, huku bomba, likipita Kitongojini hapo, kuelekea eneo la Ngega lililopo umbali wa Kilometa 2 kutoka walipo; mahali anapoishi Mwekezaji ambaye ni mfugaji, John Kalinga
Akizungumza kwa niaba ya Wanawake wa eneo la Nyakavangala, Emy Sanga amesema kuwa wao ndio wanaumia zaidi kutokana na uhaba wa maji kitongojini hapo, na kwamba Wanaume wanasubiri kupata huduma ya chakula, pasipo kujua vile maji yanavyopatikana.
Anasema hali hiyo inawafanya wakati mwingine kulazimika kujibana zaidi katika fedha za mahitaji wanazoachiwa na waume zao, ili kupata fedha ya kununua maji ya kunywa na kupikia; huku usafi wa nguo zao, ukitegemea maji ya mvua, hususan kipindi cha masika na wakati wa kiangazi, wanalazimika kuchimba maji chini, maji ambayo yana chumvi.
Aidha, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mgodini, Saleh Mohamed Sakomba amesema tatizo la maji limekuwa kubwa na kwamba, wameendelea kuiomba Serikali kusaidia kutatua tatizo hilo, kwani maji yaliyopo ni ya kisima ambayo yana chumvi.
Diwani wa Kata ya Malenga Makali, Stephano Mkisi akizungumza kuhusu Amos Sosopi kupata maji pekee yake, huku Wananchi wengi wakikosa huduma, amesema alipowauliza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazigira Iringa (IRUWASA), majibu yao yalikuwa kwamba, eneo hilo ni sehemu ya kutolea upepo baada ya maji kusafiri umbali mrefu wa zaidi ya Kilomita 12
Kwa upande wake Mkurugenzi Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Iringa (IRUWASA), Mhandisi Fabian Maganga amekanusha kumpelekea maji mwekezaji wa ufugaji umbali wa Kilomita 12, bali ni umbali wa mita 450 tu.
Hata hivyo, akizungumza nyumbani kwao, Mke Mkubwa wa Sosopi alisema hafahamu namna mume wake alivyounganishiwa maji, kutoka katika bomba kubwa lililopo pembeni ya uzio wa eneo lao