Mwekezaji wa Arsenal akana kutaka kuuza hisa zake

Mwekezaji wa Arsenal akana kutaka kuuza hisa zake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mwekezaji wa pili kwa ukubwa katika klabu ya Arsenal, Alisher Usmanov, anasema kuwa hajafanya mazungumzo yoyote na mwenye hisa mkuu wa klabu hiyo Stan Kroenke kuhusu kumuuzia kiwango chake cha hisa katika klabu hiyo.

Imeripotiwa kuwa Kroenke ambaye anamiliki asilimia 67 za hisa aliwasilisha ombi la kutaka kununua hisa za Usmanov ambazo ni asilimia 30. Hata hivyo Usmanov mwenye umri wa miaka 64 amesema kuwa maslahi yake katika Arsenal ni ya muda mrefu.

''Nadhani umiliki wangu wa asilimia 30 ni kitengo muhimu katika kulinda maslahi ya mashabiki katika klabu hiyo'', alisema.

Licha ya kumiliki hisa katika klabu hiyo Usmanov hayupo katika bodi ya klabu hiyo ambayo hufanya maamuzi na amekuwa akimlaumu Kroenke kwa matokeo mabaya ya Arsenal uwanjani. Raia huyo wa Uzebek aliwasilisha ombi la £1bn mnamo mwezi kuinunua klabu hiyo lakini likakataliwa na Kroenke.



BBC
 
Ni kibaraka wa Wenger huyu mzee team Coyg
 
Stan Kreonke huyu Mmarekani ni kiazi kweli nina mpango wa kumshitaki kwa Kim Jong Un.

Anafanya Arsenal yetu kuwa kuwa mbaya kila siku kimatokeo uwanjani.
 
Bora asiuze.. huyu kroenke ndio tatzo pia kwa arsenal
 
Back
Top Bottom