the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Mwekezaji wa vitalu vya uwindaji wa kitalii Saleh Salimu Alamry amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha akikabiliwa na Mashtaka Sitini ya Uhujumu uchumi, kughushi, kutumia Nyaraka za uongo pamoja na kuongoza Genge la uhalifu.
Mshtakiwa Namba moja ni Salehe Salum, akishtakiwa pamoja na Wakili Sheck Mfinanga, ambapo anadiwa kutumia Nyaraka za uongo kuwalaghai Wakurugenzi wenzake ambao ni Raia wa Saudia Arabia na
kujipatia hisa 18 za kampuni, Ubadhirifu wa Fedha za Kampuni Dola za Kimarekani milioni 8.
Kampuni hiyo inafahamika kama Sunset Tarangire Limited, Tawi la Al Rajhi Holding Company Limited ambayo inajihusisha na huduma za uwindaji wa kitalii nchini Tanzania.
Edgar Bantulaki ni Wakili wa Serikali Mwandamizi akiongoza jopo la mawakili wengine wa serikali, ameimbia mahakama kuwa washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Pwani na Manyara.
Vielelezo zaidi ya 400 vya vitu na Mashahidi 80 wanatarajiwa kutoa ushahidi katika kati Kesi hiyo.
Hata hivyo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwakuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo namba 24767/2024.
Kesi hiyo itasikilizwa katika Mahakama Kuu, Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi na itapangiwa Tarehe hivi Karibuni.
Jopo la mawakili wa Utetezi linaongozwa na Wakili Moses Mahuna, ambapo ameiomba mahakama kupanga mapema tarehe ya Usikilizwaji ili Haki iweze kutendeka.