Uchaguzi 2020 Mwelekeo wa Kampeni 2020 unaenda vizuri mpaka sasa

Uchaguzi 2020 Mwelekeo wa Kampeni 2020 unaenda vizuri mpaka sasa

masare

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
1,791
Reaction score
1,830
Wanajamvi,

Takribani wiki moja sasa tangu kipyenga cha kuanza Kampeni kilipopulizwa.Vyama vya siasa vipo "field" kuomba kura. Japo ni mapema mno kutoa tathmini ila so far tunaomba mambo yanaenda vizuri labda yaharibike siku za mbeleni. Zile siasa za "majitaka" pamoja na kushambulia mambo binafsi ya wagombea mpaka Sasa sijasikia kutoka upande wowote ule iwe ni chama tawala au upinzani.

Nakumbuka uchaguzi wa mwaka 2010 siasa za majitaka zilitamalaki ambapo mgombea Dr Slaa alianza kuchafuliwa kuwa eti kaiba mke wa mtu.Vivyohivyo kwenye uchaguzi mkuu uliopita mgombea Edward Lowassa aliambiwa ni "mgonjwa" .

Kwa sisi ambao hatuna ushabiki wa chama chochote tungependa Kampeni ziendelee kwenye mstari huuhuu.Tusingependa kusikia tena siasa za majitaka,porojo na kubwabwaja maneno ovyo kutoka kwa wahusika wa Kampeni.

Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom