Mwelekeo wa kupata katiba mpya

Mwelekeo wa kupata katiba mpya

andrew tezie

Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
13
Reaction score
2
Kutokana mwanzo wenye mashaka wa upatikanaji wa katiba mpya huenda Rais Kikwete akakumbukwa kwa moja wapo kati ya kuwa mwanzilish wa kupata katiba hiyo au kuanzisha mtafaruku wa kitaifa.Hii ni kutokana na jinsì CCM walivyooyesha kuwa kinyume na maoni yaliyopatikana.Sasa ukitumika hoja ya nguvu kufanya maoni ya CCM ndiyo yatumike badala ya maoni ya wadau hapo ndiyo mvutano na mfarakano utakapoanzia,mie nina mashaka sana kama tutamaliza salama zoezi hili naomba ufafanuzi.
 
Hivi na wewe unaamini Mawazo ya watu 47,820 walipendekeza Serikali tatu ndio mawazo ya Wananchi million 45?
kwa nini hudhani wale watu zaid ya 50% waliotoa maoni yao bila ya kuzungumzia Muungano maana yake wanakubaliana na hali ya serikal mbili ndio maana hawakuona haja ya kujadili muungano. Kwa namna yeyote ile Mawazo ya watu 47,820 hayawezi kuitwa mawazo ya wanachi walio wengi, tunaweza kuyaita mawazo ya watoa maoni kwenye tume ya Warioba sio Mawazo ya Wananchi wote.
 
Acha kutokwa na povu, una upofu kiasi gani hata usielewe kua watu walijikita kwenye mambo mengine yaliyopo kwenye rasimu? ulitaka wote waongelee muungano kisha masuala mengine yaachwe? haujui umuhimu wa sampling? ulitaka watu wote takribani 45m waulizwe kuhusu muungano halafu mambo mengine yaachwe? ww huo muungano una faida nao ipi zaidi ya kelele za kila siku? acha muda uongee msiwaoneshe watz cha kufanya wataamua wenyewe, halafu hii rasimu ya katiba ina kipengee cha muungano tu mbona vngne haviguswi
 
Nashukuru kwa muongozo wako.Kwa uelewa wangu mdogo nilifikir hao watu 45,000 unaotaja wamewakilisha makundi mbalimbali miongoni mwa wananchi.Ktk hili pia ningeomba unitoe hofu yangu.
 
Hivi na wewe unaamini Mawazo ya watu 47,820 walipendekeza Serikali tatu ndio mawazo ya Wananchi million 45?
kwa nini hudhani wale watu zaid ya 50% waliotoa maoni yao bila ya kuzungumzia Muungano maana yake wanakubaliana na hali ya serikal mbili ndio maana hawakuona haja ya kujadili muungano. Kwa namna yeyote ile Mawazo ya watu 47,820 hayawezi kuitwa mawazo ya wanachi walio wengi, tunaweza kuyaita mawazo ya watoa maoni kwenye tume ya Warioba sio Mawazo ya Wananchi wote.

Mimi nilidhani hao watu 47,820 wamewakilisha wananchi wa makundi mbalimbali sababu kupata maoni kutoka kwa watu 45m moja moja nadhan zoezi lingechukua karne moja kukamilika.Je kwa mtazamo huo ina maana katiba tunayosubiri haitokani na maoni ya wananchi?Kwa hali hiyo ni kwamba tunajindanganya wenyewe na kupoteza fedha bure kwa ajili ya zoezi ambalo ni batili?Naomba ufafanuzi zaidi.
 
Ningeomba tusome kitabu kinaitwa " ON THE EXAMINATION OF ONESELF" japo kimeandikwa na kiongozi mmoja wa dini kitatusaidia kufanyaaamuzi bila woga. Kufanya maamuzi kwa ajili ya watu. Kuacha kutamani kujifikiria faida binafsi ya katiba ila kufikiria faida ya kundi zima la watanzania.
Inasikisha inavyojionyesha kuwa inawezekana utashi wa wengi wa wajumbe wa bunge la katiba wamejaa woga. Wanategemea akili zao kuongea wanazima utashi wa mioyo yao unalilia kutenda mema kwa watu.
Wanasikiliza na kutimiza masharti ya akili za kibinadamu zinazoogopa vitu vya kibinadamu.
Pls soma hicho kijitabu kidogo
 
Ninakushukuru sana bwana Haika.Je naweza kupata wapi nakala ya kitabu hicho kwa sababu kusoma ni kujifunza mengi.
 
Kipate online au jaribu cathedral bookshop. Au duka la vitabu linalouza machapisho ya papa benedict
 
Back
Top Bottom