Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,089
- 2,725
- Thread starter
-
- #41
Kama wewe ndio unafanya hiyo consultation ni bora wakuache mara moja maana huna unachoelewa na umekimbilia kudesa andiko hilo moja!
Kama kweli wewe ni mtaalamu tuambie "knowledge gap" kufikia malengo husika.
Rudi kwenye SDG's uangalie mwisho ni lini kufikia lengo hilo kidunia! Hilo andiko naweza kulichambua kwa nusu saa wahusika wote mkapoteana na tukamuomba Rais mrudishe fedha za walipa kodi mlizolipwa vilaza wakubwa mliovamia field!
Queen Esther
Huwa napenda kujadiliana kwa mtindo wa point counter point ili niweze kuona wapi hoja yangu ni dhaifu na wapi hoja ya mwenzangu ni imara, halafu nifanye adjustment. Sioni kitu hicho kikitokea katika mawasiliano kati yangu nawe. Jitahidi kujielekeza kwenye hoja badala ya kushambulia mtoa hoja.
Pointi yangu ni hii: kwa Tanzania tatizo la "universal health coverage system" linatokana na vyanzo vya fedha za kuendesha mfumo huo. Ukiangalia SP ya Wizara ya Afya iliyomalizika 2020, kulikuwa na mependekezo ya vyanzo vipya vya fedha za kuendesha mfumo huu. Lakini, mpaka SP hii inafikia ukomo vyanzo hivyo havikuwa feasible. Technical Ministerial Papers zote zilizowasilishwa huko juu ziligonga mwamba. Mpaka leo hakuna waraka wa serikali unaoeleza chanzo cha fedha za kuendesha "universal health coverage system".
Any aidea on the way forward?