Mwendazake na kipenga uwanjani, nimekumbuka kauli ya kata miwa badala kupuliza kipenga. Awamu ya mwendazake panahitajika kitabu Cha somo tosha darasan

Mwendazake na kipenga uwanjani, nimekumbuka kauli ya kata miwa badala kupuliza kipenga. Awamu ya mwendazake panahitajika kitabu Cha somo tosha darasan

Fasta fasta

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2011
Posts
1,125
Reaction score
725
Wana ndugu.

Habari zenu? Nimeyasoma ya Sabaya nimesikitika sana Kama ni kweli. Kama ni kweli shutuma zinazosemwa basi watu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha tuwape pole. Lakini najiuliza alikuwa anajiamini namna gani?

Je lilikuwa ni kosa la watanzania, Katiba na sheria zilizondani yake, matumizi mabaya ya madaraka, dola kutumia nguvu kubwa kuwanyamazisha wananchi kwa ajili ya kumfurahisha bosi wao, watanzania kuwa busy na maisha yao ya Sasa badala ya kuangalia na ya wakati ujao, watanzania hawakujiajiri taliyokuwa yanatokea, n k

Je lilikuwa ni kosa la Refa au mwendazake au vipiiii. Hapo Sina shaka kwa sababu hata TRA waliingilia account za watu bank na kuzifungia. Tulisikia matamko ya UVICCM yakiwa makali kwa kujiamini. Tulisikia ya kutekwa na maiti kuokotwa Coco beach. Wengine wamepotea mpaka Sasa hawajulikani.

Bunge likawa vichekesho mpaka spika anajilaumu sheria zingine zimepitishwa tukiwa tumelala.

Haki za binadamu ikabidi ijitose kwa jicho Kali lakini ile kauli ya Refa na kata miwa ikapungua. Bado kuna mengi watu wamefanyiwa lakini walikuwa hawana mahali pakwenda kwa kutishiwa. Leo hii tunajua mama yetu Rais wetu atafungua njia watanzania wafungue macho tena na wajiamini Kama watanzania tena.

Sasa mwendazake kaondoka ila kaacha vivairas

Siwezi kuandika yote ila nashauri awamu ya mwendazake kiandikwe kitabu. Kielezee madhara ya kutokufuata sheria katika uongozi na hitaji la watanzania wa leo la katiba mpya.

Kitabu Kama kitaandikwa vizuri basi dunia inaweza kusaidia kupatikana kwa katiba mpya.

Watanzania ni waoga kwa sababu ya kauli Kama za Akina Muruto na Mambosasa na vijana wao. Watanzania wanajua gharama za kujitibu hawana Kama watajeruhiwa. Na wengi wanategewa na ndugu, familia n.k.

Hicho kitabu kichambue kila kitu serikalini hasa viongozi waliotumika awamu ya tano, kwa Jamii, bunge, taasisi n.k.
 
Nakazia: "somo liwe na msingi wa kuwa our never should be never again!"

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
𝙰𝚝𝚊𝚊𝚗𝚍𝚒𝚔𝚊 𝚗𝚊𝚗𝚒? 𝚖𝚊𝚊𝚗𝚊 𝚔𝚒𝚕𝚊 𝚖𝚝𝚞 𝚊𝚗𝚊 𝚖𝚕𝚎𝚗𝚐𝚘 𝚠𝚊𝚔𝚎 𝚔𝚠𝚊 𝚞𝚢𝚘! 𝙺𝚊𝚖𝚊 𝚖𝚒𝚖𝚒 𝚋𝚒𝚗𝚊𝚏𝚜𝚒 𝚗𝚊𝚖𝚞𝚘𝚗𝚊 𝚊𝚕𝚒𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚜𝚊𝚠𝚊 𝚗𝚊 𝚗𝚊𝚊𝚖𝚒𝚗𝚒 𝚒𝚕𝚒 𝚝𝚊𝚒𝚏𝚊 𝚕𝚒𝚜𝚘𝚗𝚐𝚎 𝚖𝚋𝚎𝚕𝚎 𝚝𝚞𝚗𝚊𝚑𝚒𝚝𝚊𝚓𝚒 𝚟𝚒𝚘𝚗𝚐𝚘𝚣𝚒 𝚊𝚒𝚗𝚊 𝚢𝚊 𝙼𝚊𝚐𝚞 𝚗𝚍𝚊𝚗𝚒 𝚢𝚊 𝚖𝚒𝚊𝚔𝚊 30 𝚝𝚞 𝚝𝚞𝚝𝚊𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚖𝚋𝚊𝚕𝚒 𝚔𝚊𝚖𝚊 𝚗𝚌𝚑𝚒, 𝚕𝚊𝚔𝚒𝚗𝚒 𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚠𝚎𝚗𝚐𝚒𝚗𝚎 𝚑𝚊𝚠𝚊𝚔𝚞𝚋𝚊𝚕𝚒𝚗𝚒 𝚗𝚊 𝚒𝚕𝚒 𝚠𝚊𝚘 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚝𝚊𝚔𝚊 𝚟𝚒𝚘𝚗𝚐𝚘𝚣𝚒 𝚠𝚊𝚙𝚘𝚕𝚎 𝚠𝚊𝚗𝚢𝚎 𝚍𝚎𝚖𝚘𝚔𝚛𝚊𝚜𝚒𝚊 𝚗𝚊 𝚖𝚒𝚌𝚑𝚊𝚔𝚊𝚝𝚘 𝚊𝚖𝚋𝚊𝚘 𝚖𝚝𝚊𝚒𝚝𝚊𝚓𝚒 𝚖𝚒𝚊𝚔𝚊 300 𝚔𝚞𝚕𝚒𝚓𝚎𝚗𝚐𝚊 𝚝𝚊𝚒𝚏𝚊 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 𝚞𝚌𝚑𝚞𝚖𝚒 𝚒𝚖𝚊𝚛𝚊.
 
Eti 2016 to 2021 wanawake 40 wabakwe na mkuu wa wilaya kisha isijulikane popote tena katika mikoa ya kaskazini?!!! Ambako kuna upinzani mkubwa kiasi kwamba hata mtendaji wa kijiji tu akifanya baya tunaliona youtube ila kwa huyu hayakujulikana mpaka alipo....... Sitaki hata kuendelea

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Kumbuka na spana ilikuwa namba ngapi? Ukiongea tu kamtata Kama huna maelezo ya kutosha weka mahabusu mpaka ajitambue.
 
Back
Top Bottom