JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Ameeleza kuwa ni kutokana na kile anachodai kuwa kesi hiyo haijakidhi matakwa ya kisheria na Kikatiba, limesikilizwa Mawakili wa Dkt. Slaa wakiongozwa na Peter Madeleka, Hekima Mwasipu, Mwanaisha Mndeme, Edson Kilatu, Paul Kisabo na wengineo wameieleza Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam ni kwa namna gani mteja wao amekuwa akisota rumande kwa muda mrefu bila kupatiwa dhamana.
Huku wakitumia jukwaa hilo kueleza wasiwasi wao kwamba huenda 'danadana' zinazoendelea kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zina 'maelekezo'.
Video: Jambo TV
Soma: Pre GE2025 - VIDEO: Dkt. Slaa ndani ya Kizimba cha Mahakama Kuu, akikabiliwa na kesi ya kusambaza taarifa za Uongo mtandaoni