Mwendesha mashtaka ICC aacha hisia tofauti kesi ya Kenyatta

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,712

Monday, September 8 2014

Taarifa iliyotolewa Ijumaa na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Fatou Bensouda kwamba, hana ushahidi wa kutosha kumshtaki Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, imewagawa waathirika wa matukio ya mauaji yaliyotokea mwaka 2007 nchini humo.

Kutegemeana na upande gani ambao waathirika hao walikuwa mwaka 2007 wakati mauaji hayo yakitokea, waathirika hao ama wamefedheheshwa au ku sikitishwa na taarifa hiyo. Wengine wametaka amani na umakini, mtandao wa standard media.co.ke umeripoti jana.

Rais Uhuru alishtakiwa kuhusiana na uhalifu uliotokea Nakuru na Naivasha kati ya Januari 24 na 28,2008 wakati mauaji ya visasi yalipotokea.

Waathirika wa uhalifu walikuwa hasa watu wa makabila ya Luona Kalenjin. Maeneo hayo mawili-Nakuru na Naivasha yalikuwa yakihifadhi idadi kubwa ya watu wa ndani waliokimbia makazi yao kutokana na kulipuka mauaji hayo ya visasi.

"Bado tunataabika kutokana na hasara tuliyopata. Kesi hiyo bado haijaleta majawabu ,"Peter Omollo ambaye alipoteza kila kitu chake eneo moja la Naivasha alikaririwa jana na mtandao wastandard media. co.ke akisema.

Alisema, waathirika wa Naivasha wanategemea kupata haki kutoka ICC sababu hakuna mashtaka yoyote ya maana yaliyofunguliwa na mamlaka kutokana na matukio ya vita hivyo vya kulipiziana visasi.

Esther Auma, kibarua mmoja jimboni humo ambaye kaka yake alikufa katika mashambulizi hayo alisema, taarifa ya mwendesha mashtaka huyo lilikuwa pigo la pili kwa waathirika hao baada ya kushindwa kupata msaada wa maana kutoka kwa Serikali ya Kenya.
"Tumesameheana kila mmoja na tunajipanga kusonga mbele, lakini hatutasahau uzoefu wetu," alikaririwa.

Hata hivyo, watu waliokimbia makazi yao kutoka kambi mbalimbali Mai Mahiu na Naivasha walikuwa na furaha namna ambavyo kesi hiyo inaendeshwa ambapo,m wenyekiti wao Stephen Mbugua alikaririw aakisema kwamba, mahakama ilikosea kwa kutohusisha watuhumiwa halisi wa mauaji hayo.

"Wakati wote tumekuwa tukisema ICC iligeuzwa mahakama ya kisiasa. Mwishowe ukweli umedhihirika," alisema.
Katika Jimbo la North Rift ambako kesi hiyo inamhusisha Makamu wa Rais, William Ruto, waathirika na viongozi walisema walikuwa na hofu zaidi kuhusu mwafaka pamoja na uwepo wa amani.

Meja John Seii, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Kalenjin, alisema kesi inayoendelea mahakamani haitaathiri utaratibu wa mazungumzo ya amani. Seii alisema utaratibu huo ulishaanza na ni lazima uendelee.

Kipokorir Menjo, Mwenyekiti wa Orange Democratic Movement (ODM) Uasin Gishu, alikubali na kusema kwamba, watu hawaelekei kuathiriwa na mwenendo wa mahakama hiyo.

"Kila mtu anaangalia mbele kufikia amani, waathirika, watuhumiwa, mwendesha mashtaka na jamii zilizoathiriwa pia.Tunatakiwa kuiachia mahakama suala hili kwa sababu ndiyo ina nafasi nzuri zaidi ya kutenda haki katika kila hali," alifafanua Menjo.

Mwakilishi wa Marakwet Mashariki, Kangogo Bowen, alielezea matumaini makubwa kwamba Rais Uhuru atasafishwa kutokana na mashtaka hayo ICC.
"Hakuna jamii ambayo haina usalama kwa wakati huu.Tunafuraha kuona kwamba, kesi zinasambaratik a," alisema.

Mbunge wa Elgeyo Marakwet, Kipchumba Murkomen, alitabiri kwamba, kesi ya Ruto itaisha kabla hata kesi ya Uhuru haijaanza.
"Hakuna hata ushahidi ulioweza kuanzishwa kesi dhidi ya Ruto. Kuna mkanganyiko mwingi sana na kujitoa (kwa mahakimu)," alikaririwa.

James Muchi na ambaye alifukuzwa kutoka Lelmolok, maeneo ya Kesses eneo la Uasin Gishu, alisema, alishagundua kwamba ICC haina uwezo wa kuendelea na kesi. Alisema kwamba, kesi hiyo haikuwa imewahusisha wahalifu halisi wa matukio hayo.

Muchina alisema kama watuhumiwa halisi wangeweza kukamatwa kesi yenye manufaa ingeweza kuendeshwa.
"Tulijua kwamba ingekuwa vigumu kupata haki wakati waathirika halisi wa tukio hawakuhusishwa kutoa ushahidi ICC," alikaririwa.

CHANZO: ​Majira
 
Monday, September 8 2014

Taarifa iliyotolewa Ijumaa na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Fatou Bensouda kwamba, hana ushahidi wa kutosha kumshtaki Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, imewagawa waathirika wa matukio ya mauaji yaliyotokea mwaka 2007 nchini humo.

Kutegemeana na upande gani ambao waathirika hao walikuwa mwaka 2007 wakati mauaji hayo yakitokea, waathirika hao ama wamefedheheshwa au ku sikitishwa na taarifa hiyo. Wengine wametaka amani na umakini, mtandao wa standard media.co.ke umeripoti jana.

Rais Uhuru alishtakiwa kuhusiana na uhalifu uliotokea Nakuru na Naivasha kati ya Januari 24 na 28,2008 wakati mauaji ya visasi yalipotokea.

Waathirika wa uhalifu walikuwa hasa watu wa makabila ya Luona Kalenjin. Maeneo hayo mawili-Nakuru na Naivasha yalikuwa yakihifadhi idadi kubwa ya watu wa ndani waliokimbia makazi yao kutokana na kulipuka mauaji hayo ya visasi.

“Bado tunataabika kutokana na hasara tuliyopata. Kesi hiyo bado haijaleta majawabu ,”Peter Omollo ambaye alipoteza kila kitu chake eneo moja la Naivasha alikaririwa jana na mtandao wastandard media. co.ke akisema.

Alisema, waathirika wa Naivasha wanategemea kupata haki kutoka ICC sababu hakuna mashtaka yoyote ya maana yaliyofunguliwa na mamlaka kutokana na matukio ya vita hivyo vya kulipiziana visasi.

Esther Auma, kibarua mmoja jimboni humo ambaye kaka yake alikufa katika mashambulizi hayo alisema, taarifa ya mwendesha mashtaka huyo lilikuwa pigo la pili kwa waathirika hao baada ya kushindwa kupata msaada wa maana kutoka kwa Serikali ya Kenya.
“Tumesameheana kila mmoja na tunajipanga kusonga mbele, lakini hatutasahau uzoefu wetu,” alikaririwa.

Hata hivyo, watu waliokimbia makazi yao kutoka kambi mbalimbali Mai Mahiu na Naivasha walikuwa na furaha namna ambavyo kesi hiyo inaendeshwa ambapo,m wenyekiti wao Stephen Mbugua alikaririw aakisema kwamba, mahakama ilikosea kwa kutohusisha watuhumiwa halisi wa mauaji hayo.

“Wakati wote tumekuwa tukisema ICC iligeuzwa mahakama ya kisiasa. Mwishowe ukweli umedhihirika,” alisema.
Katika Jimbo la North Rift ambako kesi hiyo inamhusisha Makamu wa Rais, William Ruto, waathirika na viongozi walisema walikuwa na hofu zaidi kuhusu mwafaka pamoja na uwepo wa amani.

Meja John Seii, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Kalenjin, alisema kesi inayoendelea mahakamani haitaathiri utaratibu wa mazungumzo ya amani. Seii alisema utaratibu huo ulishaanza na ni lazima uendelee.

Kipokorir Menjo, Mwenyekiti wa Orange Democratic Movement (ODM) Uasin Gishu, alikubali na kusema kwamba, watu hawaelekei kuathiriwa na mwenendo wa mahakama hiyo.

“Kila mtu anaangalia mbele kufikia amani, waathirika, watuhumiwa, mwendesha mashtaka na jamii zilizoathiriwa pia.Tunatakiwa kuiachia mahakama suala hili kwa sababu ndiyo ina nafasi nzuri zaidi ya kutenda haki katika kila hali,” alifafanua Menjo.

Mwakilishi wa Marakwet Mashariki, Kangogo Bowen, alielezea matumaini makubwa kwamba Rais Uhuru atasafishwa kutokana na mashtaka hayo ICC.
“Hakuna jamii ambayo haina usalama kwa wakati huu.Tunafuraha kuona kwamba, kesi zinasambaratik a,” alisema.

Mbunge wa Elgeyo Marakwet, Kipchumba Murkomen, alitabiri kwamba, kesi ya Ruto itaisha kabla hata kesi ya Uhuru haijaanza.
“Hakuna hata ushahidi ulioweza kuanzishwa kesi dhidi ya Ruto. Kuna mkanganyiko mwingi sana na kujitoa (kwa mahakimu),” alikaririwa.

James Muchi na ambaye alifukuzwa kutoka Lelmolok, maeneo ya Kesses eneo la Uasin Gishu, alisema, alishagundua kwamba ICC haina uwezo wa kuendelea na kesi. Alisema kwamba, kesi hiyo haikuwa imewahusisha wahalifu halisi wa matukio hayo.

Muchina alisema kama watuhumiwa halisi wangeweza kukamatwa kesi yenye manufaa ingeweza kuendeshwa.
“Tulijua kwamba ingekuwa vigumu kupata haki wakati waathirika halisi wa tukio hawakuhusishwa kutoa ushahidi ICC,” alikaririwa.

CHANZO: ​Majira

Kamata raila hapo ndo kutakuwa na kesi
 
Back
Top Bottom