Mwendokasi kusitisha tiketi za karatasi kuanzia Machi, wasafiri kutumia kadi janja

Mwendokasi kusitisha tiketi za karatasi kuanzia Machi, wasafiri kutumia kadi janja

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART Mwendokasi ) umesema kuanzia mwezi March mwaka huu wa 2025 utasitisha rasmi matumizi ya tiketi za karatasi katika usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka na badala yake Watumiaji wote wa Mabasi watatakiwa kutumia kadi janja ambazo zinaendelea kuuzwa katika vituo vikuu vya mradi huo.

1738910800658.png

Akiongea Jijini Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha mradi wa Maendelezo Yatokanayo na uboreshaji wa usafiri wa umma (TOD), Mtendaji Mkuu wa DART Dkt. Athumani Kihamia amesema ifikapo tarehe mosi mwezi March matumizi ya tiketi za karatasi katika kulipia nauli za mwendokasi yatasitishwa.

"Ni kweli tumeendelea kusisitiza Watumiaji wa Mabasi yetu ya Mwedokasi wajitahidi kuwa na kadi janja na kuzitumia lakini hata hivyo baadhi yao bado hawatumii kadi hizo, napenda kusisitiza kuwa ifikapo tarehe mosi mwezi March mwaka huu tutasitisha kabisa matumizi ya tiketi za karatasi ili wasafari wote wanaotumia Mabasi ya Mwendokasi watumie kadi"

1738913920963.png
Amesema matumizi ya kadi yanaondoa usumbufu wa kukosekana kwa chenchi lakini pia ni njia muafaka ya kudhibiti uvujaji na upotevu wa mapato ya Serikali.

Soma: Mchengerwa: DART Hakikisheni Wakazi wa Dar es Salaam Wanapata Kadi Janja za Mabasi ya Mwendokasi
 
Back
Top Bottom