Mwendokasi wa madereva wa magari ya umma

Mwendokasi wa madereva wa magari ya umma

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Wengi ni mashahidi jinsi magari ya umma hasa za Serikali yanavyoendeshwa kwa kasi bila hatua yeyote kuchukuliwa. Magari kama V8, Landcruiser hardtop yanaendeshwa kwa spidi inayozidi kilomita 200 kwa saa huku askari wa barabarani akisimama pembeni mwa barabara na kuangalia tu na hata kuipigia gari saluti kama kuna mkubwa ndani.

Balaa inakuja gari ya fusso ikipita mbele ya traffic itasimamishwa na kuulizwa maswali kumi kidogo na faini juu. Ajali ya jana isingetokea kwa maelezo ya RPC Simiyu kama dereva wa Serikali asingekuwa kwenye mwendo kasi. Nashauri wote tuheshimu sheria ya barabara uwe mkubwa Serikalini au raia wa kawaida.
 
Mabosi zao ndo wanataka hvyo ukiwa slow kazi huna.
 
Back
Top Bottom