Mwenendo huu wa biashara hata siuelewi!

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
14,834
Reaction score
32,522
Wadau nipo kwenye biashara ya Hardware mwaka wa pili sasa, mwanzo biashara ilikuwa poa mpaka nikawa najisemea biashara ndiyo hii!

Hali imechange sana mwaka huu japo mwaka jana hali ilianza kudorola taratibu, sasa mwaka huu hata kipindi ambacho huwa tunaona ni cha biashara mambo yamekuwa sio kabisa!

Kwakweli stress nilizonazo hazielezeki, mzigo umejaa dukan wateja hakuna mtu unakomaa kwa siku unaondoka na elf 20.

Hapa nawaza niswitch kwenda kwenye biashara gani nashindwa kuelewa!

Vipi huko wenzetu hali ya biashara ikoje, mtu asije akaniambia niingie Forex hiyo naifahamu tayari!
 
Mkuu hakuna biasha “tangible” ambayo leo inalipa vzr. Zote maumivu tu. Wengne mpaka tunajikuta tunasusua maana unaamka asubuh unaenda kufanya biashara unarud jion km ulivyoenda bora ww unarud na 20. Kiukweli mambo si mazur na mwenye macho aone..hii sio siasa ni life reality.
 
Vyuma mkuu. Ukweli ni kwamba watu hawana pesa. Mie na store ya vyakula lakini mauzo ni ya ajabu. Mtu unauza shs 800000 kwa siku wakati tulishazoea 5000000 kwa siku!

Tafuta grees mkuu. Vyuma hivyo
 
Ukilima unasubiri mvua tu hakuna wa kumlaumu labda sr God achelewe kufungulia bomba na visima vikauke
 
Biashara n ngumu mno tuseme tu ukweli mm moja nishafunga tin no kabisa sikutaka kuja kusumbuana na tra ,,hali n tete mno ....walau waajiriwa wanauhakika na amount yao mwisho wa mwezi wafanyabiashara tuko hoi bin taaban huwez sema unakopa ukawa na uhakika wa kulipa kabisa
 
Mbaya zaidi ukiwa na mkopo benki afu mwisho wa mwezi unatakiwa kurudisha marejesho hapo ndio utajuta kuwa mfanyabiashara.....

Ila all in all huu ni upepo yote yatapita na mambo yatarudi kuwa kama yalivyokuwa mwanzo...
 
Mbaya zaidi ukiwa na mkopo benki afu mwisho wa mwezi unatakiwa kurudisha marejesho hapo ndio utajuta kuwa mfanyabiashara.....

Ila all in all huu ni upepo yote yatapita na mambo yatarudi kuwa kama yalivyokuwa mwanzo...
True
 
ndugu zangu msikate tamaa kwani hiki ni kipind cha mpito tu maana hakuna mfanya biashara asie lalamika kwani Tanzania yetu biashara asilimia kubwa tunamtegemea mkulima, Na msimu huu inaonesha kutakuwa na neema sana kwani hali ya mazao sio mbaya hivyo kuanzia April ni neema tu.
 
Shukuru Mungu kwakila jambo,kama Kipindi cha nyuma Ilikua Poa usikate tamaa komaa biashara Kuna kupanda na kushuka
 
Shukuru Mungu kwakila jambo,kama Kipindi cha nyuma Ilikua Poa usikate tamaa komaa biashara Kuna kupanda na kushuka
Ni kweli mkuu, lakini kwa hali iliyopo sioni unafuu ukipatkana mapema!!
 
Kipindi km hiki ni kigum kwa kweli,ila mm nimezoea biashara ya mazao hapa naomba Mungu bei za mahindi zipande.maana mpunga tunashukuru na hizi krismass.

~pia naomba we unaiamuru asubuhi yako sawasawa na ayubu 38:12.

~Usiingie kichwa kichwa kwenye duka lako.mkabidi Bwana,achilia damu ya Yesu,itakase bishaya kwa damu ya Yesu,mwambie Mungu afungue pande za nchi.

~Ombea ardhi ya duka lako,ina masikio inasika,teka nyanra za hiyo ardhi na uachilie damu ya Yesu sawasawa na waebrania 12:24.

~Amuru malaika waondoe kila udhaifu sawasawa na zaburi 91:11
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…