Mimah0005
New Member
- Aug 14, 2022
- 1
- 1
Maana halisi ya elimu
Elimu ni tendo la uzoefu wenye athari ya kujenga akili tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi,vile vile tunaweza kusema elimu ni mafunzo tunayopata kutoka kwa watu wengine ili kukuza maarifa yetu juu ya ulimwengu unaotuzunguka vile vile elimu hukuza fikra zetu maadili yetu,pamoja na kutufunza sheria mbalimbali muhimu. kuna aina kuu mbili za elimu ambazo ni elimu rasmi na elimu isiyo rasmi.
Elimu rasmi- hii ni elimu inayojumuisha elimu kabla ya kuingia kwenye soko la ajira na ni elimu inayotolewa kwa kufuata utaratibu maalumu wa ufundishaji uliopangwa kitaifa, elimu hii inajumuisha elimu ya ufundi ,elimu ya mahitaji maalum na elimu ya watu wazima pia elimu hii hutolewa na walimu wenye sifa maalum ambao wanapaswa kuwa na ujuzi katika sanaa ya kufundisha pia inazingatia nidhamu kali.
Elimu isiyo rasmi –hii ni elimu inayopatikana kwa njia isiyo na muundo nje ya taasisi za elimu za jamii.hii inahusisha dhana ambazo hupatikana katikaa mfumo wa maisha ya kila siku kama kazi burudani na mawasiliano na watu wengine,mafunzo haya hayahusishi kuhitimu wala upatikanaji wa vyeti.
kwa miaka ya hivi karibuni inaonekana kuwa elimu ya tanzania imeboreka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na miaka iliyopita mabadiliko haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya teknolojia na utandawazi vile vile uongozi bora na uanzilishi wa sera bora zinazoihusisha hasa sekta ya elimu mfano baada ya hayati rais Dr. john pombe magufuli kuingia madarakani alipitisha sheria ya elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka sekondari ili kusaidia upatikanaji wa elimu kwa urahisi na kupunguza gharama za elimu kwa wazazi, sheria hii imesaidia pia kupunguza ongezeko la watoto wa mitaani ,ndoa za utotoni na ajira kwa watoto vile vile serikali kwa kiasi fulani imeweza kutatua matatizo mbalimbali yaliyokua yakihusisha mila potofu katika jamii na yaliyokua yakimkandamiza mtoto wa kike kwa kutoa vipaumbele vya elimu kwa watoto wakike nchini.
Historia ya elimu ya tanzania kwa ufupi
Historia ya elimu ya Tanzania imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni:elimu kabla ya uhuru na elimu baada ya uhuru.
Elimu kabla ya uhuru
Tangu apo zamani hata kabla ya uhuru kulikua na utoaji wa elimu kwa njia tofauti tofauti pia elimu kabla ya uhuru ilihusisha aina mbalimbali za elimu kubwa ilikuwa ni elimu ya jadi ambayo ilikuepo kabla ya kuja kwa wageni katika mwambao wa tanganyika ambapo kila kabila lilikua namfumo wake wa utoaji wa elimu ya kijadi elimu hiyo ilijumuisha maarifa, stadi, maadili na utamaduni,elimu wakati wa ukoloni ni elimu iliyotolewa na wageni wa kwanza tanzania bara ambao walikua ni waarabu,wakifuatiwa na wareno,wajerumani,na waingereza
Elimu baada ya uhuru
wizara ya elimu iliundwa kama chombo kinachojitegemea mwaka 1960,mh oscar kambona akiwa waziri aliyehusika na elimu kwa kipindi chake chuo kikuu cha daressalaam kilianzishwa na usawa ukaanza kuzingatiwa katika kuchagua wanafunzi wa kuingia sekondari bila kujali rangi, kiswahili kilianza kutumika kufundishia hadi darasa la tano na kupanuliwa hadi darasa la nane mnamo mwaka 1968 baada ya hapo darasa la nane lilifutwa na kubaki madarasa saba ya elimu ya msingi yaliyopo hadi leo.
vile vile mnamo mwaka 1967 kulipitishwa azimio la arusha na mfumo wa elimu ya kujitegemea ili kujenga dhana ya udadisi,kujenga uwezo wa kujitegemea kutoka kwa wengine na kutathmini ya wengine ,kujifunza kufikiri na kuchambua mambo,kujenga uwezo wa kujiamini na kujikomboa kimawazo na kujitegemea.
Faida za elimu kwa watanzania
Elimu kwa watanzania inafaida nyingi zikiwemo;
1.Kuboresha pato la taifa
Pato la taifa GDP linaboreka kutokana na kuimarika kwa idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika.hivyo katika jamii kukiwa na idadi kubwa ya watu walioelimika wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi kulingana na taaluma zao na kupelekea kuongezeka kwa pato la taifa kama jambo la maendeleo ,na kama tunavyojua maendeleo ya taifa yanategemea zaidi jamii ya wasomi.
2 .kupunguza kiwango cha uhalifu
Wananchi wakipata elimu sahihi kiwango cha uhalifu katika taifa hupungua.kwakua watu watakuwa wanafahamu vizuri sheria na madhara ya uvunjaji wa sheria.
3. Kujenga mazingira ya kizazi kijacho cha wataalamu kustawi
Utoaji wa elimu kwa kizazi kilichopo husaidia kwa kiasi kikubwa uimarikaji wa kizazi kijacho na hujenga misingi imara ya uelimikaji wa kizazi kijacho.
4. kufunza maadili katika jamii
katika jamii yeyote kukiwa na watu walioelimika uvunjwaji wa maadili na utovu wa nidhamu huwa kwa kiasi kidogo maana mambo mengi ya nidhamu hufundishwa katika sekta mbalimbali za elimu, ivyo basi katika jamii kukiwa na watu wengi walioelimika hata ukiukwaji wa maadili na haki za binadamu unaweza kuwa kwa kiasi kidogo sana.
5. Kutatua matatizo katika jamii
kwenye jamii iliyo na watu walioelimika kunakuwa nauwezekano mkubwa wa utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii maana matatizo yanaweza kutatuliwa kwa kufuata sheria na nidhamu ya hali ya juu hivyo kupelekea kujengeka kwa jamii imara
Pamoja na yote yanayochangia uimarikaji wa elimu nnchini tanzania bado kuna changamoto zinazoikumba sekta ya elimu nchini ambazo ni pamoja na;
1. masilahi mabovu ya walimu, nchini taanzania sekta ya elimu haizingatiwi sana kama sekta nyingine japokuwa inajulikana kuwa elimu ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi ,tunaona katika nchi yetu mishahara ya walimu iko chini sana na haikidhi matakwa ya maisha ya sasa na walimu wanazidi kukandamizwa siku hadi siku.
2. ubovu wa mitaala ,mitaala ya elimu nchini haiendani na wakati tuliopo bali mitaala inayotumika hadi sasa ni ya zamani na haikidhi viwango vya elimu ya sasa maana sasa dunia ipo kwenye utandawazi lakini elimu yetu haiendani na hali halisi ya ulimwengu wa sasa.
3. mfumo wa elimu yetu hauendani na mfumo wa elimu ya dunia ya sasa,ni kweli kwamba mfumo wa elimu yetu inayotolewa nchini hauendani kabisa na mfumo wa elimu ya dunia kwasababu mfumo wa elimu wa sasa unahitaji matumizi ya teknolojia kwa kiasi kikubwa lakini tanzania bado hatujafikia kiwango icho na bado tunatumia mfumo wa elimu wa zamani.
4. kutokuwepo kwa uwajibikaji , hili pia nitatizo kubwa linaloikumba sekta ya elimu nchini kwa maana kuwa wazazi na wadau mbalimbali wa elimu wamekua hawawajibiki ipasavyo katika kutekeleza mambo mbali mbali yanayoihusu sekta ya elimu na wamekuwa hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa walimu ili kujua matatizo mbalimbali mashuleni na kuyatatua kwa pamoja kama ikiwezekana,
Nini kifanyike ili kupunguza na kuondoa kabisa mapungufu yaliyopo katika sekta ya elimu tanzania?
kwanza:serikali inatakiwa kuwatizama kwa jicho la tatu walimu kwa kuwajali kwa kiasi kikubwa kama vile kuwaongezea mishahara, kuwajengea nyumba bora za kuishi wao na familia zao vile vile kuwapatia masilahi bora mara baada ya kustaafu.
Pili:serikali inatakiwa kuboresha mitaala ya tanzania ili iendane na soko la elimu ya sasa maana mitaala inayotumika sasa ni ya zamani na iliyopitwa na wakati na siyo rafiki kwa ulimwengu huu wa kiteknolojia.
Tatu: wadau wa elimu na wazazi kwa ujumla wao wanatakiwa kuipa kipaumbele sekta ya elimu kwa kijumuika pamoja katika shughuli mbali mbali za kielimu kama vile kuchangia katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya shule na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi mashuleni, kwa kufanya hivyo tunaweza kujenga kizazi bora cha wasomi katika taifa ambao pia wanatarajiwa kuwa wajenzi bora wa jamii zetu na taifa kwa ujumla
Hitimisho, pamoja na yote niliyoainisha hapo juu serikali inalo jukumu kubwa la kuhakikisha elimu inayotolewa nchini inakidhi vigezo vya soko la ajira kwa sasa na technolojia iliyopo kama hayati rais magufuli alipopitisha tamko la' Tanzania ya viwanda' na kuendelezwa na rais wa sasa wa tanzania mama samia suluhu hassan; kama tunavyojua kuwa nguvukazi kubwa ya taifa ni vijana hivyo serikari inahitaji kuwatengeneza vijana walioelimika watakaoweza kutekeleza sera hii kwa ufasaha zaidi ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii na kuchochea maendeleo ya nchi kwa ujumla na hayo yote yatatekelezwa endapo tu sekta ya elimu itaboreshwa kuendana na matakwa ya jamii na kuendana na mfumo wa elimu wa dunia
Ahsanteni!

Upvote
2