Mwenendo wa soko la nyumba Dar es Salaam

Mwenendo wa soko la nyumba Dar es Salaam

DarProperty Tz

Senior Member
Joined
Apr 24, 2011
Posts
168
Reaction score
29
Bei za Masaki,Oysterbay, Nyumba za Biashara, Mikopo ya nyumba kuporomoka.
Bei za Kigamboni, Mikocheni, Kijitonyama, Msasani kupanda.


Karibu mwaka 2015, mwaka huu Tanzania inategemea kushuhudia matukio makubwa mawili. Kupiga kura ya maoni kwa katiba mpya na uchaguzi mkuu. Kwa upande wa umiliki wa ardhi (real estate) inategemewa kupata msisimko zaidi. Utabiri huu umelenga maeneo saba (7).

Utabiri wa kwanza; Viwango va mikopo ya nyumba kushuka.
Mwaka 2014 mikopo ya nyumba ilipanda mpaka kufikia 16.5%- 20%. Mwaka 2015 mikopo ya nyumba inategemewa kushuka mpaka 13%-17%. Tutarajie kuongezeka kwa wadau wengine angalau wanne (4) watakao toa mikopo hivyo kuongeza ushindani. Hali hii pia itachangiwa na msukumo wa upatikanaji wa mikopo kutoka kwa kundi ushirika (affiliated group). Pia shinikizo kwa serikali kuratibu matumizi na ukopeshaji wake hivyo kupelekea uwepo wa fedha kwenye taasisi za kifedha za kukopesha jamii.

Utabiri wa pili; Bei za nyumba.
Kutakuwa na mabadiliko ya bei katika sehemu mbalimbai jijini Dar es Salaam.
Watakaonufaika:
Baada ya Masasani kufanya vibaya mwaka 2014. Bei za makazi Msasani inategemewa kupanda baada ya maboresho ya miundombinu hasa uboreshaji wa njia za majitaka na barababra ndogo zinazoingia mitaani. Uharibifu uliofanywa na mafuriko ya 2014 utakuwa historia, mafuriko hayo yaliwafukuza wapangaji wengi na kuwa kisingizio kwa wanunuzi wapya kutotaka kuhamia.
Mikocheni ipo katikati ya miradi miwili mikubwa, mradi wa Kawe Uptown wa NHC uliopo Kawe Beach, pia mradi wa eneo la kibiashara wa Mara Group lenye ukubwa unaokaribia eneo la futi mraba milioni 3.5 lililopo jirani na ubalozi wa Marekani. Miradi hiyo itaisaidia Mikocheni kuwa eneo linalotafutwa zaidi kwa ajili ya biashara na makazi.
Kunduchi, Mbezi na Tegeta itapata ongezeko la mahitaji hivyo ongezeko la bei baada ya upanuzi wa barabara ya Bagamoyo kurahisisha usafiri wa wakazi wa maeneo hayo.
Tumeshuhudia Kijitonyama ikibadilika kutoka eneo la makazi na kuwa eneo jipya la kibiashara hususani sambamba na barabara kuu kuelekea bagamoyo.
Masaki, Oysterbay na Upanga. Kwa miaka mingi maeneo haya yalifaidi bei za juu katika soko la upangaji lakini hali imeanza kubadilika. Tutashuhudia bei zikishuka katika maeneo hayo kwa sababu ya msongamano wa makazi. Ukweli usiopingika maeneo haya yalikuwa maeneo yaliyotafutwa zaidi na watu wa kipato cha juu, lakini hivi karibuni wapangaji wamepata maeneo mengine mazuri kwenye sehemu tofauti. Kwa mwaka 2014 pekee imepata nyongeza ya nyumba 1000, huku ujazo wa mahitaji (absorption rate) kwa mwaka 65%.

Utabiri wa tatu: Bei za Kigamboni.
Tumesikia mengi kuhusu eneo hili hatimaye yametimia. Japo serikali haijachukua hatua madhubuti za moja kwa moja lakini sekta binafsi na waendelezaji (developers) wameishachukua hatua. Daraja la Kigamboni lililowezeshwa na mfuko wa NSSF linatarajiwa kukamilika July 2015, litasaidia sana kurahisisha usafiri hivyo tutegemee ongezeko kubwa la bei.
Dege Eco Village, Avic town na shule ya michezo ya Real Madrid itakuwa kichocheo kikubwa cha ongezeko la bei kwani wanunuzi wanahakikishiwa kupata mahitaji ya kijamii yote ndani ya eneo moja.

Utabiri wa nne: Tusitegemee uwekezaji mpya mkubwa.
Mwaka 2014 tulishuhudia mambo mengi mapya. Mwaka huu tusitegemee mambo mapya. Wawekezaji wengi husubiria kuona mwelekeo wa uchaguzi na hupeleka fedha zao kusaidia washirika wao wa kisiasa.

Utabiri wa tano: Bei za nyumba za biashara kushuka.
Siku za neema kwa majengo ya biashara zinaonekana kuelekea ukingoni. 2015 tutashuhudia poromoko la bei katika sekta hii. Hii imesababishwa na ubadilishwaji wa makazi binafsi kuwa nyumba za biashara na ongezeko kubwa la majengo ya kibiashara. Katika kipindi cha upanuzi, usambazaji(supply) unakuwa mdogo kupelekea uhitaji kuwa mkubwa hivyo bei za upangaji kupanda. Mwaka 2015 usambazaji/ugavi (supply) utapanda kutokana na ongezeko la majengo mapya mwaka jana. 2014 soko lilikuwa na zaidi ya mita za mraba 65,000 kwenye maeneo ya kitega uchumi ambayo hayajapata wapangaji. Wakati inategemewa nyongeza ya mita za mraba 100,000 kujengwa na kasi ya kujaza nafasi umefikia 46%. Habari njema kwa sasa majengo mengi yanawapangaji kwa 70%, utabiri unaonesha kutakuwa na msinyao wa soko kwa walau 12% kwa mwaka huu.

Utabiri wa sita: Uingiaji wa makampuni na Chapa za kimataifa yanayojihusisha na umiliki ardhi sokoni.
Chapa ya Knight Frank ilianza kuwekeza nchini 1994, ukifuatiwa na chapa ya Regus na mwaka jana tukashuhudia chapa kutoka marekani ya Remax yakiingia sokoni. Mwaka huu tutegemee angalau makampuni mawili zaidi ya kimtaifa kujiingiza katika soko hili (real estate).

Utabiri wa saba: Matumizi ya teknohama.
Utafutaji wa nyumba au viwanja kwa miaka mingi ulikuwa kwa njia ya taarifa za mdomo kupitia marafiki/ ndugu, na ilifanyika kwa kwenda na kujionea mwenyewe. Sekta ya umiliki wa ardhi (real estate) haijabaki nyuma nayo inatumia teknohama kurahisisha huduma kwa wauzaji na wanunuzi kwa kutumia tovuti na simu za mikononi. Mwaka 2015 Darproperty imeamua kuanzisha uombi wa simu ya mkononi (mobile application) mbili kwa ajili ya simu za kawaida na smart phone ambazo zitabadilisha jinsi watu wanavyotafuta nyumba, kupata taarifa za soko, kulinganisha nyumba ili kufanya maamuzi sahihi kwa watu wote wanaopenda kufatilia masuala ya sekta hii.
Kuanzishwa kwa maombi hati miliki kupitia mtandaoni.
Mbunge wa Kigoma Mh. Zito Zuberi Kabwe hivi karibuni alitoa mapendekezo bungeni juu upatikanaji wa hati ya kwenye mtandao. Alipendekeza kama njia ya kumaliza migogoro ya ardhi nchini. Mh. Zito alisema hayo wakati akichangia ripoti ya mwaka ya bunge ya Kamati ya Ardhi, Mazingira na Maliasili bungeni Dodoma. Kwa ushawishi wake wa kushinikiza ajenda tunaweza kushuhudia utekelezaji wake ukitokea mapema zaidi ya ilivyotarajiwa na kuvuma zake ndai ya mwaka 2015.


Kufahamu zaidi kuhusu soko la nyumba, tembelea tamasha la kimataifa. fuata link hapo chini.
The DarProperty Expo 2014
https://www.facebook.com/events/813707358684907/
 
Nnaamini taarifa hii na kwa muda nilihisi hivyo. Ila naona mmedeal na the high class real estate sub market pengine tunahitaji study kwa the lower sub market ambayo ina actors wengi
Na wenye impact kubwa kiuchumi kwa taifa.all the same lovely effort.
 
Nnaamini taarifa hii na kwa muda nilihisi hivyo. Ila naona mmedeal na the high class real estate sub market pengine tunahitaji study kwa the lower sub market ambayo ina actors wengi
Na wenye impact kubwa kiuchumi kwa taifa.all the same lovely effort.
any economy is driven by middle income class! hata mtoa mada analenga kundi hilo hilo!
 
Nnaamini taarifa hii na kwa muda nilihisi hivyo. Ila naona mmedeal na the high class real estate sub market pengine tunahitaji study kwa the lower sub market ambayo ina actors wengi
Na wenye impact kubwa kiuchumi kwa taifa.all the same lovely effort.

Tunatanguliza shukrani! Tutayafanyia kazi mapendekezo yako kadri muda na hali itakapo ruhusu.
 
Nimependa sana utabiri na hizo taarifa
 
Back
Top Bottom