KERO Mwenendo wa uendeshaji wa treni ya Tabora-Mpanda

KERO Mwenendo wa uendeshaji wa treni ya Tabora-Mpanda

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakuu Naomba mnisaidie kupaza sauti kwa Serikali ifanye marekebisho kwenye reli ya Tabora-Mpanda hali ni mbaya mno, Yaani treni imekuwa na huduma za Hovyo Mno, unaandikiwa kwenye ticket treni litafika saa tisa mchana ila cha ajabu treni linafika saa Tatu usiku.

Kwa ufupi wananchi wa huku wanalalamika sana kutokana na uchakavu wa reli. Wewe fikiria sehemu ya 190km treni linatembea Masaa 13 Mpaka 14. Hiki kitu nimekutana mara Mbili nimepanda treni kwa mara ya kwanza ila sitamani tena kupanda.

Serikali iangalie namna bora ya kuboresha Hii reli

Soma Pia:

~Treni ya Abiria ya TRC yaanguka Kigoma, Watu kadhaa wajeruhiwa
~ Treni ya Dar-Tanga-Arusha imekwama, wanaohusika watoe mwongozo wa nini kinaendelea



image.jpg

 
Back
Top Bottom