Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Kwamba unaweza kumwambia mtu kuwa unampenda bila kuhofia kuwa utakataliwa, yaani hauwazi kabisa cha muhimu kwako unampenda mtu huyo,yaan haijalishi kama yeye atakupenda bali cha msingi ni wewe kumpenda yeye.
Kitu kingine unawakubali watu jinsi walivyo, haijalishi wana mapungufu gani, haijalishi ni wakorofi kiasi gani,haijalishi ni ndugu wa karibu au mbali, marafiki au majirani.
Upo tayar kutoa msaada kwa unayemjua na usiye mjua maadamu ni wanadamu wenzako,upo tayar kutoa msaada kwa anayeomba na asiyeomba maadamu unajua kuwa ni wahitaji na wanapaswa kusaidiwa.
Unawasalimia watu hata kama wewe hawajakusalimia,haijalishi unawafahamu au huwafahamu,ni majirani au wapita njia,,maadamu ni binadamu wemzako wewe unashow love.
Upo tayar kutenda haki,iwe kwa matajiri na maskini,iwe kwa wakubwa au wadogo,iwe kwa wenye hadhi zao na wasio na hadhi,maadamu ni binadamu wenzio na wanastahili usawa katika maisha.
Umejaaaliwa kipato kizuri,maisha bora,unavaa utakacho na kula utakacho,unaishi sehemu nzuri lakini huna majivuno,haudharau watu,upo mkarimu na mpole kwa watu wote
Umejaaliwa upeo mkubwa wa utambuzi,una hekima na busara pia,una maarifa mengi sana lakini unapenda kusikiliza mawazo ya watu wengine,unapenda kujifunza kutoka kwa watu wengine,na upo tayar kukosolewa pale unapokosea.
Najaribu kuwaza mambo mengi sana lakini mda hautoshi
Ni hayo tu!