Mwenendo wote wa kesi ya Lissu Alhamisi, Septemba 24, 2026

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
SEHEMU YA KWANZA

[Mshtakiwa TAL anaingia Mahakamani.]

[Majaji wanaingia.]

KARANI: Criminal Session, Kesi Na. 19605 ya 2025, Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.

LISSU: Nipo tayari, Mheshimiwa Jaji.

JAJI NDUNGURU: Tuendelee.

LISSU: Nashukuru. Naomba kwanza nikumbushwe niliishia wapi.

JAJI NDUNGURU: Ulisema unamaliza kwenye sheria, unaanza kuzungumzia ushahidi sasa. Unakumbuka?

LISSU: Waheshimiwa Majaji, nashukuru. Kabla sijaendelea na ushahidi, naomba nizungumzie kitu kimoja muhimu ambacho Mahakama hii ilipata kusema kwenye kesi ya Freeman Aikael Mbowe.

Kuto kufafanua essential elements kwenye hati ya mashitaka.

Mahakama hii, katika kesi ya Freeman Aikael Mbowe, ilikuwa inajadili kushindwa kwa upande wa mashitaka ku-disclose mamlaka halali.

Mamlaka halali maana yake ni nini?

Mahakama hii ilisema katika ukurasa wa 53 wa hukumu:

«“Statutes must give fair notice or warning to those subject to them. They must guard against arbitrary and discriminatory enforcement and they must not reasonably…”»

Sheria zinatakiwa kutoa tahadhari sahihi kwa wale wanaotegemewa kuzifuata. Ziwalinde watu dhidi ya mamlaka holela au matumizi holela ya madaraka yanayotumiwa na sheria, na sheria zisinyime watu uhuru wa kuzungumza. Isipowalinda wote, tutakuwa wafungwa.

Mahakama ilisema yafuatayo kuhusu sheria za aina hii:

«“Such statutes must be under the doctrine of overbreadth.”»

«“If the statute is so overbroad written that could deter free speech then it can be struck down because of its chilling effects.”»

Maana ya Overbreadth Doctrine ipo katika Black’s Law Dictionary, toleo la saba.

Kesi ya Freeman Aikael Mbowe ilimalizia kwa maneno haya, ukurasa wa 58:

«“The failure to lay a name of lawful authority targeted by utterances prejudice the first accused, upon which it can evaluate if the word in question were calculated to achieve the act or conduct said to be seditious. The charge was defective.”»

Kwa kifupi, hati ya mashitaka inayosema alichochea umma.

Wasafiri, wasiosafiri, wageni, wenyeji, watoto wachanga, hao wote ni umma.

Huwezi kujitetea kwa hati ya namna hiyo.

Ndiyo maana Mahakama imesema haya maneno yafafanuliwe katika hati ya mashitaka.

Yasipofafanuliwa, hayo mashitaka ni batili.

Hati imeingiza neno “umma” ambalo halipo katika sheria na, pili, haijalifafanua.

Kwa sababu hiyo, ni hati ya mashitaka batili.

Waheshimiwa Majaji, baada ya kujibu hivyo, naomba sasa nijibu maswali niliyoacha jana.

Ukiachilia mbali ubatili wa namna hiyo, je, ushahidi wao unasemaje?

Waheshimiwa Majaji, hapa nazungumzia ushahidi unaohusu nia ya kuchochea umma iliyoletwa na wanaonishitaki.

Ushahidi kuhusu nia ya kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Na hiyo nia haipo katika sheria.

Je, ushahidi unasemaje kuhusu hiyo nia ya kuzuia umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana?

Waheshimiwa Majaji, jambo la kwanza kabisa ni kwamba katika mashahidi 17 wa upande wa mashitaka waliotoa ushahidi kwa kiapo mbele yenu, Waheshimiwa Majaji, ni mashahidi wanne tu ndiyo waliotoa ushahidi kuhusiana na suala hili.

Mashahidi hao ni:

PW1, ACP George Byagemu;

PW2, Inspector John Kaaya;

PW16, Assistant Commissioner of Police Amin Mahamba;

na PW17, shahidi wa gizani.

Hao ndiyo waliotoa ushahidi wa mimi kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu.

Jambo la pili katika ushahidi huu, watatu kati ya hao mashahidi wanne ni polisi. Mmoja tu, PW17, ndiye ambaye si polisi.

Watatu kati ya hao wanne hawakuwepo katika huo mkutano. Hawakuhudhuria.

Mmoja tu, PW17, ndiye aliyekuwapo katika mkutano.

Waheshimiwa Majaji, PW17 ni shahidi pekee katika mashahidi wote 17 ambaye ni eye witness. Ndiye aliyekuwapo na aliyesikia.

Wengine wote hawakuona wala kusikia yaliyozungumzwa. Waliona tu mambo ya mtandaoni.

Huyo PW17 si tu aliona na kusikia, ndiye aliyerusha matangazo.

Sasa hii inahusu suala ambalo lipo mbele yenu, ambalo ninatuhumiwa kwamba mimi ndiye niliyerusha matangazo ambayo yanadaiwa kuwapo katika mtandao wa Jambo TV.

Waheshimiwa Majaji, kesi ya upande wa mashitaka imejengwa kwenye nini?

Kesi ya upande wa mashitaka imejengwa katika ushahidi wa PW1, PW2 na PW16.

Dhana ya kesi hii ni kwamba mimi, mshtakiwa, nilichochea umma kwa kuzungumza maneno yale yaliyo katika hati ya mashitaka kwa lengo la kuitishia Serikali kwa sababu moja tu.

Kwamba hii Serikali ndiyo inayosimamia sheria za nchi hii.

Then uchunguzi unaendeshwa na Katiba na sheria.

Kujaribu kuzuia uchaguzi unazuia Serikali inayosimamia sheria hizo.

That’s their theory. That’s the entire basis ya hii kesi.

Sasa hii nadharia imetokana na ushahidi wa hawa polisi watatu.

Tuanze na PW1, George Wilbert Bagyemu.

Waheshimiwa Majaji, PW1 ndiye aliyepewa taarifa kwamba kuna video yenye maneno ya kijinai.

Ndiye aliyepewa taarifa kwamba kuna maneno katika mtandao wa Jambo yenye jinai.

Alipelekewa na PW2 siku ya tarehe 4 Aprili 2025, siku moja tu baada ya huo mkutano.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, PW1 alisema nini juu ya hii nia ya kuchochea umma kuzuia uchaguzi na kwa hiyo kutishia Serikali?

Maneno yake yapo katika ukurasa wa 146 wa rekodi.

Anazungumzia kipi kilichomfanya aamini kuna kosa la uhaini.

«“The factors which led to conclude that’s it was treason offence.”»

«“Where the accused words that ‘atahamasisha uasi, atazuia uchaguzi, atavuruga sana, atakinukisha sana sana, atavuruga sana, atakinukisha vibaya sana.’”»

Hicho ndicho kilichomfanya askari polisi Byagemu ajue huu ni uhaini.

Anaendelea kusema, kwa maoni yake, kwa alivyoona:

«“These words were communicated with the intention to threatening the executives.”»

«“I say so because the election is held as per Constitution and laws.”»

Ataendelea kusema:

«“The executive enforces the law. He intimidated the Executive for the purpose of violating the law…”»

Kwa hiyo, kesi yote ipo hapa.

Ukitaka kuzuia uchaguzi, umeitishia Serikali. Kwa nini? Kwa sababu Serikali ndiyo inasimamia sheria.

Haya yapo katika ukurasa wa 146.

Waheshimiwa Majaji, mtakumbuka kwamba PW1 was subjected to cross-examination.

Kwenye cross-examination, PW1 alikiri kwamba katika hayo maneno anayolalamikia hakuna maneno “Serikali”, wala “Serikali ya Jamhuri ya Muungano”, wala “Serikali ya Mapinduzi Zanzibar”. Wala hakuna maneno Rais Samia Hassan Suluhu, hakuna maneno Isdory Philips Mpango, hakuna maneno Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam au Albert Chalamila.

Kwa maneno yake katika ukurasa wa 157, amesema hiyo Serikali anayodai imetishiwa haipo na viongozi wake wote hawapo.

Hakuna jina la kiongozi yeyote wa Serikali lililotajwa katika hiyo kauli ya kihaini.

Hayo ni kukiri kwake katika cross-examination.

Pamoja na yote, PW1 continued to insist that was intended to threaten the Government.

Akasema yafuatayo katika ukurasa wa 166 wa rekodi:

«“When a person says ‘Kukinukisha sana’ umetenda uhaini.”»

Akaendelea kusema:

«“The words ‘Kukinukisha sana’, ‘Kukinukisha vibaya sana sana’ are not in Penal Code 39(2)(d).”»

Isipokuwa uliyasema umefanya kosa la uhaini kwa sababu gani? Kwa sababu Serikali ndiyo inayosimamia uchaguzi.

LISSU: Huo ndiyo ushahidi, Waheshimiwa Majaji, unaowashawishi mtoe hukumu ya kunyonga mtu. Hawana hata aibu.

JAJI NDUNGURU: Tuendelee na submission hiyo. “Hawana hata aibu” haina haja.

LISSU: Waheshimiwa Majaji, I am entitled to show them nimeumizwa sana kwa maneno haya. Nimekaa ndani mwaka mmoja na nusu.

JAJI NDUNGURU: Tuendelee.

LISSU: Waheshimiwa Majaji:

«“The evidence of records suggests strongly…”»

Alipoamua kwamba huu ni uhaini, hakuna kitu chochote ambacho kingebadilisha mawazo yake.

Mfano, alipohojiwa PW17, aliyekuwa shahidi wa kuona na kusikia, wala hakuona tatizo lolote katika maneno yote yaliyozungumzwa.

PW1 akasema yafuatayo kwenye ukurasa wa 166:

«“It’s true that in his statement P said you were discussing challenges facing you in your constituencies. He also said you were wearing up the police of No reform No election. It was me who ordered the opening of the treason file.”»

Nimesoma maelezo yake nikaamua kufungua kesi ya uhaini. Ni mimi ndiye niliyeamua kufungua kesi ya uhaini baada ya kusoma maelezo yake.

Waheshimiwa Majaji, maelezo ya PW17 ambayo PW1 anasema aliyasoma hayajasema kwamba kuna kosa lolote, achilia mbali la uhaini.

So nothing was going to change him.

Alipoulizwa na Mawakili wa Serikali, re-examination, akaulizwa: unasemaje juu ya hayo maneno? Je, yanahusu Serikali ya Jamhuri ya Muungano?

Ukurasa wa 176 akasema:

«“Maneno yaliyonukuliwa katikati ya hati ya mashitaka kwa mukhataza wake yanahusu Serikali.”»

Mukhataza ni interpretation.

Alirudia maneno yale yale kwamba uchaguzi unaendeshwa kwa Katiba na Serikali ndiyo inasimamia sheria.

Kwa vile uchaguzi unaendeshwa kwa sheria na Katiba na Serikali ndiyo inasimamia hiyo sheria, maneno “Serikali” hayapo ila yapo.

Kisichokuwapo kinaingizwa constructively.

Waheshimiwa Majaji, huo ni ushahidi wa PW1.

Alipotoa ushahidi huo huo, ndiyo ukawa ni msimamo wa kila polisi aliyekuja kutoa hapa ushahidi.

Waheshimiwa Majaji, PW2 alisema yafuatayo wakati anaongozwa katika ushahidi wake, ukurasa wa 183:

«“Maneno ya ‘tutaenda kuzuia uchaguzi’, ‘kuhamasisha uasi’ yana viashiria vya jinai.”»

Kwa hayo maneno niliyaona yanaashiria jinai.

Kwa sababu uchaguzi unaendeshwa kwa Katiba na sheria.

Kuzuia uchaguzi bila amri ya Mahakama ni kiashiria cha jinai.

Kwa sababu kuzuia uchaguzi unaosimamiwa na sheria na sheria inasimamiwa na Serikali.

Ukurasa wa 183.

Msimamo wa PW2 ulikuwa ni msimamo uleule wa PW1.

PW16, polisi mwingine.

Waheshimiwa Majaji, mtakumbuka PW16 ndiye aliyechukua nafasi ya uongozi wa timu ya George Byagemu, ukurasa wa 444.

«“The accused intended to intimidate the Government…”»

«“The conduct of intimidating the Government by threatening to obstruct the General election… amounted to treason.”»

Kitendo cha kutishia Serikali kwa kuitishia kuzuia uchaguzi kwa kuhamasisha uasi kilikuwa ni uhaini.

Waheshimiwa Majaji, PW16 akaendelea kuelezea kwa nini haya maneno ni uhaini, ukurasa wa 445:

«“The words used by the accused such as ‘tutazuia uchaguzi’, ‘tutahamasisha uasi’ were intended to intimidate the Government which is vested with responsibility to protect the Country.”»

Kwa hiyo, kujaribu kuzuia uchaguzi ni uhaini.

Uchaguzi ni kwa mujibu wa sheria. Uhaini wa maneno tu.

Waheshimiwa Majaji, under re-examination, PW16 baada ya kukaa muda mrefu kwenye cross-examination, anasema hivi katika ukurasa wa 485 na 486:

«“What I meant [is] that the Government is authority responsible to implement and enforce the laws.”»

Huo ndiyo ushahidi wa polisi waliotoa ushahidi.

Msimamo wao ndiyo huo: ukitishia uchaguzi tu ni uhaini.

That is police thinking and not legal thinking.

Waheshimiwa Majaji, si kila shahidi wa upande wa mashitaka alikuwa na msimamo huo.

Shahidi namba 17, the eye witness.

Kitu muhimu cha kuanzia hapo, PW17 haungi mkono hiyo theory ya polisi.

Ni shahidi pekee katika hao mashahidi 17 aliyepinga ushahidi wa mashitaka.

Kwenye ushahidi wake, ushahidi wake ni tofauti completely.

PW17 alisema kuhusu lengo la mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025:

«“That meeting was intended to bring together CHADEMA aspiring candidates to discuss the slogan of No Reform No Election.”»

Akaendelea kusema:

«“A lot has been discussed in that meeting.”»

Akasema:

«“However, the main issues included the slogan No Reform No Election.”»

«“I recall they stated that without electoral reform they will not participate in general election.”»

Ukurasa wa 491 wa rekodi, Waheshimiwa Majaji. Hayo ni maneno ya aliyekuwapo, aliyesikia, aliyeona na aliyesambaza mtandaoni.

Na, Waheshimiwa Majaji, PW17 was also extensively cross-examined.

Kama aliona au kusikia lolote kuhusu uhaini.

Nilipomuuliza, wewe uliyekuwapo, uliona chochote cha uhaini?

Akasema kwamba:

«“It’s true that in my statement I did not state in Exhibit D16…”»

Ni kweli kwenye maelezo yangu ya maandishi sikusema kwamba maneno yaliyozungumzwa na Tundu Lissu ni kosa au ni maneno ya kihaini.

Sina hakika kwamba taarifa tulizorekodi zinaweza kufikiriwa kuwa za kihaini.

Sikusambaza maneno ya kihaini, sikuandika maneno ya kihaini kwa sababu sikuona uhaini.

Waheshimiwa Majaji, Kielelezo D16 ni muhimu sana, maelezo ya PW17.

Waheshimiwa Majaji, Kielelezo D16 kipo kimya kabisa kuhusu maneno “tutakinukisha”, “tutahamasisha uasi”, “tutavuruga” sijui nini na nini.

Hayapo kabisa kwa shahidi huyu wa upande wa mashitaka.

Maelezo haya yapo ukurasa wa 497 na 498. Anasema hivi:

Hayo maneno hayapo kwenye Kielelezo D16. Ni kweli kwamba nilikuwapo katika mkutano.

Anasema viongozi hawakukosea kuzungumzia changamoto wanazokutana nazo wakati wa uchaguzi.

Na huyu ni shahidi wao. Angekuwa wa kwangu wangesema, “Unategea nini?”

Waheshimiwa Majaji, Kifungu cha 67(1) cha Sheria ya Ushahidi kinazungumzia ushahidi wa moja kwa moja.

Hicho kifungu huwa kinaitwa the best evidence.

Kama ni ushahidi wa kuona, ni shahidi wa kuona.

Kama ni wa kusikia, ni shahidi aliyesikia.

PW17 ni the best witness.

LISSU: Wameniweka gerezani mwaka mmoja na nusu wakijua sina hatia kwa maneno ya shahidi wao.

Nisipozungumza haya kwa ukali, Waheshimiwa Majaji, mawe yatazungumza.

Waheshimiwa Majaji, PW17 alikuwa shahidi wa mafichoni na mimi nina shida sana na hilo kwa sababu ninaamini sana open justice.

Lakini, Waheshimiwa Majaji, in all fairness, huyu ni shahidi bora aliyetoa ushahidi wake mafichoni.

Huyu hakukamatwa na Polisi kama wale wengine ambao walikamatwa, wakashitakiwa na baadaye wakafutiwa kesi ili waje kutoa ushahidi kwa Tundu Lissu.

Muhimu zaidi kuhusu shahidi huyu, ushahidi wake unaunga mkono ushahidi wote wa utetezi.

On all major questions, Waheshimiwa Majaji, PW17 amepingana na ushahidi wa Prosecution.

Waheshimiwa Majaji, kwa hilo mashahidi wanne wa mashitaka wametofautiana fundamentally.

Maana yake ni kwamba kuna ndimi mbili na effect ya hizi ndimi mbili.

Na hili nilisema jana, Waheshimiwa Majaji, ni suala la kufa na kupona.

Without proof, kesi inakufa.

Waheshimiwa Majaji, ninachotaka kusema hapa ni kwamba kesi yote ya mashitaka imejengwa kwenye hisi.

Ukizuia uchaguzi uliowekwa kisheria, maana yake umeitishia Serikali.

Waheshimiwa Majaji, je, ni kweli kwamba Serikali ndiyo chombo pekee kinachosimamia sheria nchi hii?

Kwenye nchi kuna kitu kinaitwa Judiciary Act. Je, sheria ya usimamizi wa Mahakama inasimamiwa na nani? Inasimamiwa na Mahakama, si Serikali.

Waheshimiwa Majaji, kuna sheria inaitwa Judiciary Act, inasimamiwa na nani? Inasimamiwa na Mahakama.

Waheshimiwa, kuna sheria inaitwa Parliamentary Powers and Immunity Act, inasimamiwa na nani? Inasimamiwa na Bunge.

Nchi hii kuna sheria inaitwa National Assembly Act, sheria ya usimamizi wa Bunge. Inasimamiwa na Bunge.

Nchi hii kuna sheria inaitwa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani. Inasimamiwa na nani? Inasimamiwa na Tume. Je, Tume ni Serikali?

Kuna Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi ya mwaka 2024. Inasimamiwa na nani? Inasimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Nchi hii kuna sheria inaitwa Kanuni za Kudumu za Bunge, inasimamiwa na nani? Na Bunge.

Kuna sheria inaitwa Sheria ya Chama cha Mawakili, inasimamiwa na Chama cha Mawakili (TLS).

Hii dhana kwamba sheria zinasimamiwa na Serikali is nonsense.

Mtu mmoja tu, polisi, kusema kwamba sheria zote zinasimamiwa na Serikali ndiyo leo tupo hapa.

It’s nonsense.

JAJI NDUNGURU: Tuendelee na submission.

LISSU: Waheshimiwa Majaji, nina haki ya kukasirika kwa sababu nimekaa gerezani kwa mwaka mmoja na nusu.

Waheshimiwa Majaji, msimamo huo uliungwa mkono na kesi za Nathaniel Alphonce Mapunda v. Jamhuri, 1006 TLR, pages 3 and 5, Mahakama ya Rufani.

Pia katika uamuzi wa Mahakama hii, kesi ya Justine Rutahirwa v. Burchard Kalumuna, Consolidated Criminal Appeal Number 7, High Court Appeal of Bukoba, 2020.

Kuhisi kwamba mtu ana lengo la Serikali, hata kama hisia ni nzito kiasi gani, haiwezi kumtia mtu hatiani kwenye kesi ya murder.

Waheshimiwa Majaji, kesi hii si ya murder, ni kesi ya uhaini.

Na uhaini ni kosa pekee lililotajwa katika Katiba yetu.

Uhaini, kama unavyofafanuliwa na sheria, ndiyo utakuwa kosa kubwa kuliko yote.

Waheshimiwa Majaji, walionishitaki wanataka mnihukumu kifo kwa sababu ya hisia yao.

Waheshimiwa Majaji, kwa msingi huu wa sheria, haiwezi kuwakubalia.

Msiitikie wito wao wa kutaka kuninyonga hadi kufa kwa sababu tu wanahisi.

Msiitikie wito wao.

Waheshimiwa Majaji, ushahidi wangu wa utetezi unasemaje juu ya hii hoja?

Waheshimiwa Majaji, kwenye ushahidi wangu, was simple, straightforward and consistent.

Ushahidi wangu wa DW1 upo ukurasa wa 589 hadi 590.

Waheshimiwa Majaji, mtaona huo wito wa ushahidi wangu:

«“Was intended to bring together, it was called with intention of kuitisha watia nia na kuwaeleza slogan ya chama kuhusu No Reform No Election.”»

Nilisema hivi:

«“In that discussion I did not refer to the Government or say what intended to do to the Government.”»

«“The allegation that we intended to threaten the Government is misplaced.”»

«“My purpose was to explain the aspirant candidates.”»

«“There was no intention to threaten the Government because it’s not part of my agenda.”»

«“I did not engage people or mobilise them…”»

I was extensively cross-examined.

Lakini hakuna Wakili wa Serikali aliyeniuliza juu ya nia yangu juu ya mkutano ule.

That testimony remained completely unchallenged.

Mahakama ya Rufani katika kesi zote tatu:

Justice Rumina Katiti (Supra);

Nyerere Nyangue (Supra);

Kiberiti (Supra).

Has established that failure to cross-examine the material is…

Kushindwa kuhoji jambo maana yake umekubaliana nalo.

Upande wa mashitaka kushindwa kunihoji nia yangu maana yake wameikubali.

Ukurasa wa 166 wa rekodi mtaona vile vile kwamba DW2 was viciously cross-examined, lakini hakubadili msimamo wake.

Mtaona ukurasa wa 691 wa rekodi.

Waheshimiwa Majaji, mtaona pia DW3 alishughulikiwa kweli kweli, lakini hakuyumba katika suala la nia, ukurasa wa 791.

Na shahidi mwingine ni DW4, Brenda Rupia, ukurasa wa 795.

Pia kwa DW5, John Wegesa Heche, mtaona kwenye kurasa za 881/882 za rekodi.

Hawakuhoji kwa sababu walikubali msimamo wetu.

Waheshimiwa Majaji, naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo kwenye hoja hii.

Nimeshitakiwa kwa kutengeneza nia ya kuchochea umma wakati Sheria ya Kanuni ya Adhabu 39(2)(d) haitambui nia ya kuchochea umma.

Nimeshitakiwa, Waheshimiwa Majaji, kwa nia ya kuchochea umma usiotambuliwa na sheria ili kutishia umma ambao haujatajwa kwenye sheria.

Nimeshitakiwa kuchochea umma usiotambuliwa kisheria kwa lengo la kutishia Serikali ambayo haijatajwa popote na hawajaleta ushahidi wa kuthibitisha hilo.

Nimeshitakiwa kwa hisia na kuleta mashitaka ya hisia.

Katika mazingira hayo, Waheshimiwa Majaji, hili suala la tatu jibu lake ni HAPANA.

That is to say, the accused person did not form any intention to obstruct the 2025 General Election to intimidate the Executive of the United Republic of Tanzania.

Kwa kutumia kesi ya Khatibu Gandi na Grey Kungu Mataka, naomba Mahakama itupilie mbali mashitaka haya kwa mujibu wa Kifungu cha 39(2)(d).

Mashitaka walipaswa wathibitishe uhaini katika kesi hii.

Waheshimiwa Majaji, nimemaliza suala la tatu. Naomba niende katika suala la nne.

Suala la nne ni: Je, hayo maneno yaliyotamkwa na mshtakiwa yanatengeneza kosa lolote linalotambuliwa na sheria za nchi hii?

Kama hayo maneno hayatambuliki kwa mujibu wa sheria, hayawezi kuwa kosa.

Waheshimiwa Majaji, suala hili lilijitokeza kutokana tuhuma ya upande wa mashitaka wakati wa preliminary hearing.

Kwamba hayo maneno yaliyosemwa yalikuwa ni kosa la jinai.

Ukurasa wa 131, Waheshimiwa Majaji.

Wakaona haya maneno yanatengeneza kosa, wakapeleka kwa ZCO na ZCO akatuleta hapa.

Tuhuma inasema hivi: Kwamba katika mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025, mtuhumiwa alidhihirisha nia yake ya kihaini kwa kusema na kuchapisha maneno yafuatayo.

Wanasema kitu kimoja sahihi hapa. Wanasema hivi, “msimamo huu unaashiria uasi.” Ni kweli. Ni kweli tunaenda kuhamasisha uasi, tunaenda kukinukisha vibaya sana.

Waheshimiwa Majaji, hakuna mahali popote ambapo upande wa mashitaka wamefafanua haya maneno.

Kwamba kuvuruga uchaguzi maana yake ni nini? Hawajasema kuhamasisha uasi ni nini na kwa nini ni kosa.

Hawajasema kuzuia uchaguzi ni nini na kwa nini ni kosa.

Hawajafafanua kukinukisha ni nini na kwa nini ni kosa.

Waheshimiwa Majaji, si wajibu wangu mahali popote.

Si wajibu wangu kisheria.

Ni wajibu wa upande wa mashitaka kufafanua hayo maneno yana maana gani na kufafanua kwa nini hayo maneno ni kosa.

It’s the question of burden of proof.

The prosecution bears the burden of proof and it never shifts.

Na hawajafafanua hayo maneno. Wameleta hisia juu ya hayo maneno.

Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa upande wa mashitaka wa haya maneno upo katika ukurasa wa 146 kwa PW1, 183 hadi 184 kwa PW2 na ukurasa wa 444 hadi 446 kwa PW16.

Waheshimiwa Majaji, mashahidi wote watatu hawa, without exception, wamesema haya maneno yanatengeneza kosa la uhaini.

Wametoa sababu zilezile kwamba maneno hayo ni uhaini kwa sababu ni polisi walewale.

Waheshimiwa Majaji, mashahidi wa utetezi wote wamesema maneno hayo si kosa kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

Kwa DW1, ukurasa wa 596 na 623.

Kwa DW2, zipo ukurasa wa 671 hadi 672, 679, 681, 699–700, 703, na 726 hadi 728.

Kwa DW3, ushahidi wake upo ukurasa wa 747 hadi 750, 753 hadi 754, 787 na 797.

Kwa DW4, ushahidi wake upo kwenye kurasa za 805 hadi 806, 810 hadi 811, 814, 818 na 831.

Kwa DW5, ushahidi wake upo kwenye kurasa za 889 hadi 890, 930 na 932.

Waheshimiwa Majaji, mashahidi wote wa utetezi wamedai kwamba hayo maneno yanayodaiwa ni ya uhaini hayana kosa kwa sheria ya Tanzania.

Waheshimiwa Majaji, kwa sababu kuna pande mbili za ushahidi zinazopingana, je, upi ni msimamo wa sheria katika jambo hili?

Mahali pa kuanzia ni katika Ibara ya 28(4), na maneno yote ya Katiba katika ibara hii ni muhimu.

Uhaini, kama unavyofafanuliwa na sheria, utakuwa ni kosa la juu kabisa.

Waheshimiwa Majaji, uhaini kwa nchi hii ni ule uliofafanuliwa na sheria, na nje ya sheria ni maneno matupu.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, kwa vile uhaini unatakiwa ufafanuliwe na sheria, ni sheria ipi inafafanua?

Ni Kifungu cha 39 ndiyo kinafafanua.

Kifungu cha 39 ni kifungu muhimu sana katika kesi hii.

Kama ninayotuhumiwa kuyafanya hayapo katika kifungu hiki, hakuna uhaini hapo; ni maneno matupu.

Kifungu cha 39 kina vipengele vinne.

Kuna matendo 10 ambayo yametajwa kama uhaini:

1. Ni kumuua au kujaribu kumuua Rais, 39(1).

2. Kuendesha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano, 39(1)(b).

Waheshimiwa Majaji, tunaingia 39(2). Kuna matendo manne ambayo ukitenda unakuwa umetenda uhaini.

3. Kutengeneza nia ya kuwezesha au kusababisha mtu au kikundi kumjeruhi Rais, kumpa kile Rais, kumjeruhi Rais; huo ni uhaini.

4. Kutengeneza nia ya kuwezesha au nia ya wengine kuwezesha kusababisha Rais apinduliwe kwa njia zisizo halali kutoka katika nafasi yake ya Urais, au kumtoa nafasi yake ya Amiri Jeshi Mkuu, 39(2)(a).

5. Ukitengeneza nia ya kuwezesha mtu au kikundi kusababisha au kuwezesha kulimdukiwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, 39(2)(c).

6. Ukitengeneza nia ya kuwezesha au kutengeneza nia ya mtu kuwezesha au kikundi cha watu kutishia Bunge au Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kosa mengine yapo kwenye 39(3):

7. Ukijiunga au kujishirikisha na maadui wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au ukawapa kinywaji au chakula maadui wa Jamhuri, 39(3)(a).

8. Kuchochea mtu yeyote kuivamia nchi ya Jamhuri ya Muungano kwa silaha. Mfano, ukileta M23 Tanzania ni uhaini, 39(3)(b).

9. Mtu yeyote atakayechukua silaha ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa lengo la kuilazimisha mambo dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Tanzania, 39(3)(c).

10. Mtu yeyote aliye na utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisaidia maadui wa Jamhuri ya Muungano kwa lengo la kuzuia shughuli za kijeshi au kuhatarisha maisha katika operesheni za kijeshi, 39(3)(d).

Sasa, Waheshimiwa Majaji, kama hayo ndiyo uhaini kama ilivyotafsiriwa na sheria:

Tuanze na “tutavuruga uchaguzi”.

Ipo wapi katika hayo yaliyofafanuliwa na Kifungu cha 39 cha Kanuni ya Adhabu?

Twende kwenye “tutazuia uchaguzi”. Haipo. Si constructively.

Twende kwenye “tuhamasisha uasi”. Ipo wapi?

Kwa Kiingereza ni rebellion, ama kama ambavyo tulisomewa katika kamusi, kupinga jambo kwa nguvu.

Twende kwenye “kukinukisha”. Ipo wapi?

Ili walau leo wanangu, wherever they are, wajue baba yao yupo gerezani kwa mwaka mmoja na nusu, baba yao kuna kosa kafanya. Haipo.

Waheshimiwa Majaji, kwenye haya ya sheria yapo wapi? Hayapo.

Nimefungwa mwaka mmoja na nusu kwa uonevu.

Nimeonewa.

Nina ndugu hapa wanakuja kila siku hapa, nimefungwa.

Nina wanachama hapa wanakuja kutoka kila mahali. Mbunge wao, Mwenyekiti wao, nimefungwa, nipo gerezani.

[Watu wanalia.]

Nalindwa na askari kama vile mimi ni muuaji. Kwa kosa gani?

Waheshimiwa Majaji, kama haya, hapo ugomvi hapa ni uchaguzi.

Tulitaka kuzuia uchaguzi, tulitaka kuvuruga uchaguzi.

JAJI NDUNGURU: Twende break.

LISSU: Sawa, Mheshimiwa.

JAJI NDUNGURU: Upande wa mashitaka?

JOB MREMA: Hatuna pingamizi, Mheshimiwa.

JAJI NDUNGURU: Bado sana kuwasilisha.

LISSU: Siwezi kusema nikajifunga. Nisije kufanya mambo kwa hisia.

JAJI NDUNGURU: Basi tuta-break kwa saa moja na nusu. Tutarudi hapa saa 8:30.

[Majaji wanatoka.]

---

SEHEMU YA PILI

[Mahakama imerejea.]

[Lissu ameingia pamoja na Majaji kupitia mlango tofauti.]

JAJI NDUNGURU: Naomba tuendelee.

NASSORO KATUGA: Iwapendeze Waheshimiwa Majaji, kolamu ipo kama awali, isipokuwa Ajuaye Zegeli amepata dharura, hatokuwapo. Mshtakiwa yeye yupo. Tupo tayari kuendelea, Waheshimiwa.

LISSU: Waheshimiwa Majaji, mimi nipo tayari.

[Lissu anapanga vitu vyake.]

JAJI NDUNGURU: Tuendelee.

LISSU: Waheshimiwa Majaji, nilipo-break nilikuwa nimependekeza tuingie kwenye hoja ya Sheria ya Uchaguzi.

JAJI NDUNGURU: Sheria ya Uchaguzi...

LISSU: Kama nilivyosema, kosa la uhaini kama lilivyofafanuliwa katika Katiba si kosa ninaloshitakiwa nalo kwenye Kanuni ya Adhabu. Kanuni ya Adhabu ni sheria pekee ambayo imefafanua kosa la uhaini.

Kwa hiyo, haya matendo ambayo nimeshitakiwa nayo hayafiti katika sehemu yoyote katika moja wapo ya matendo 10 ambayo kifungu cha 39 kimeyataja kwamba ukiyafanya haya utakuwa umefanya kosa la uhaini.

Maana yake ni kwamba mimi sijafanya kosa lolote la uhaini, lolote.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, kama sijafanya kosa lolote la uhaini, je, nimefanya kosa lingine lolote kwa mujibu wa sheria za Tanzania?

Ndicho ninachotaka tujadili.

Waheshimiwa Majaji, maneno ninayolalamikiwa hapa ni maneno yanayohusu uchaguzi, kuzuia uchaguzi, kuvuruga uchaguzi, uchaguzi, ndiyo ulikuwa unalalamikiwa hapa.

Je, hayo maneno ni makosa kwa mujibu wa sheria za Tanzania?

Waheshimiwa Majaji, jibu la swali hili linajulikana kupitia Sheria Na. 1 ya Mwaka 2024 ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Waheshimiwa Majaji, sheria hii ndiyo iliyotumika kwa mara ya kwanza katika yale maafa ya Oktoba 29 mwaka jana. Ilitungwa kwa ajili ya uchaguzi wa 2025 uliokuwa ufanyike, badala yake ikawa maafa kuliko maafa yote tangu Vita ya Majimaji, kwa mujibu wa taarifa ya DW Radio.

Je, sheria hii inayatambua kama ni makosa ya jinai?

Waheshimiwa Majaji, jibu lipo kwenye Sura ya Saba ya sheria hiyo ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Sura ya Saba, Waheshimiwa Majaji, kichwa chake cha habari ni “Makosa na adhabu zake”.

“Makosa yanayohusu uchaguzi na adhabu zake.”

Waheshimiwa Majaji, sheria hii katika Sura ya 7 imeorodhesha jumla ya makosa 23 na adhabu zake.

Kuanzia kifungu cha 114 hadi kifungu cha 136 ni orodha ya makosa na adhabu zake.

Makosa ambayo ukiyatenda unaweza kushitakiwa na ukafungwa au ukapewa adhabu nyingine za kijinai.

Maneno ambayo tunataka kuyajua ni makosa ni: “Tutahamasisha uasi”, “tutavuruga uchaguzi”, “tutazuia uchaguzi”.

Yale yote ambayo yamekuwa yakiimbwa, “uhaini, uhaini, uhaini, uhaini”.

Uzuri wa sheria hii imeandikwa kwa Kiswahili.

Waheshimiwa Majaji, kosa la kwanza lipo kifungu cha 114 cha sheria hii. Linaitwa “Makosa yanayohusu uandikishwaji wa wapiga kura”.

Lipo kwenye kuvuruga uchaguzi? Kuzuia uchaguzi? Kuhamasisha uasi? Halipo.

Kosa la pili linaitwa “Kutumia wadhifa kushawishi watu wengine wasiteuliwe kuwa wagombea”.

Nimeshitakiwa nalo? Hakuna.

Hilo la pili lipo kifungu cha 115. Halihusu kuzuia uchaguzi.

Kosa la tatu ni “Mwenendo usiofaa wa Mtendaji wa Uchaguzi”.

Mimi si Mtendaji wa Uchaguzi, halinihusu.

Kosa la nne ni “Makosa yanayohusu Daftari la wapiga kura na kadi za wapiga kura”.

Linahusika kwenye haya mashitaka? Halihusiki.

Lipo kifungu cha 119 cha sheria.

Kosa la 5 ni “Mwenendo usiofaa wa Maafisa Wandikishaji”, kifungu cha 120.

Mimi sikuwa Afisa Mwandikishaji.

Kosa la 6 ni kosa linalohusu fomu za uteuzi au karatasi za wapiga kura.

Kosa la 7 lipo kifungu cha 122 cha sheria, linahusu matangazo ya uongo ya kujitoa.

Sijashitakiwa kwa hilo, sihusiki.

Kosa la 8 ni “Vishawishi vya rushwa kwa ajili ya kujitoa”.

Hilo vilevile sihusiki nalo.

Waheshimiwa Majaji, kwenye kifungu cha 124 inasema “Makosa Mengineyo”.

Ina kifungu kinasema kutoa tamko la uongo katika chaguzi.

Sijashitakiwa kwa kutoa tamko la uongo.

Waheshimiwa Majaji, kosa la 9 linahusu utunzaji wa siri. Kuna siri nyingi wanaosimamia uchaguzi, kuna siri nyingi.

Ukivujisha hizo siri, kwa mujibu wa kifungu cha 125, ni kosa.

Kosa la 10 ni katika kifungu cha 126, “Kosa la Hongo, Takrima au Kurubuni mtu”.

Kwa hiyo, sihusiki.

Kosa la 11 ni Impersonation (kujifanya mtu mwingine).

Unachukua kadi ya mwenzako, unajifanya wewe ndiyo yeye.

Halinihusu.

Kosa la 12 linaitwa “Kupoteza sifa kwa kuhukumiwa kwa kosa la kitendo cha rushwa au kufanya matendo haramu ya kiuchaguzi”.

Kosa la 14, Waheshimiwa Majaji, lipo kifungu cha 129 kwa watu wanaodaiwa kuwa na ushawishi mbaya.

Sijashitakiwa kwa kuwa na bad influence.

Kosa la 15 lipo kifungu cha 130, “Hongo, rushwa kwa maafisa wa Tume”.

Sijashitakiwa kwa kuhonga maafisa wa Tume.

Kosa la 16 ni hatia ya kujifanya mtu mwingine.

Mimi ni Tundu Lissu wa siku zote, halinihusu.

17 ni vitendo vya rushwa na haramu, hilo halinihusu.

18, “Kuingilia mikutano halali ya hadhara ya kampeni”.

19 ni makosa yanayohusu siku ya uchaguzi. Kuvaa nguo za chama siku ya uchaguzi ni kosa. Kufanya kampeni siku ya uchaguzi, sijashitakiwa nayo vilevile.

Kosa la 20 ni “Unyanyasaji wa Kijinsia katika uchaguzi”.

Hilo nalo halinihusu katika kesi hii.

Kosa la mwisho la 21 linaitwa “Kuchafua matangazo ya uchaguzi”.

Wagombea wanaweka picha, wewe unaenda kuzirarua.

Waheshimiwa Majaji, hayo ndiyo makosa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.

Hakuna kuzuia uchaguzi, si kosa.

Hakuna kuvuruga uchaguzi, si kosa.

Hakuna kuhamasisha watu kufanya uasi, si kosa.

Hakuna kukinukisha, si kosa.

Si kosa, Waheshimiwa Majaji.

Kifungu cha 5 kinasema kosa ni kitendo au jaribio au kutenda kitu ambacho sheria imekiwekea adhabu.

Kama sheria haijakitamka, si kosa.

Hayo maneno ambayo yanadaiwa ni ya kihaini si kosa kwa mujibu wa kifungu cha 39 chote.

Na vilevile si kosa kwa mujibu wa makosa yaliyoorodheshwa Sura ya Saba katika Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Huwezi kuchochea kitu ambacho hakijakazwa na sheria.

Huwezi kuchochea jambo halali.

Unachochea jambo haramu.

Waheshimiwa Majaji, sasa nataka nifunge hoja yangu kwenye hiyo issue, suala.

Na je, hayo maneno yanayolalamikiwa ni makosa kwa mujibu wa sheria?

Hayo maneno si makosa kwa mujibu wa kosa la uhaini wala sheria nyingine ya nchi hii.

Jibu la issue namba 4 ni HAPANA.

Maneno yanayolalamikiwa si makosa yanayotambuliwa na sheria za Tanzania, let alone treason.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, naomba kwa ruhusa yenu niende kwenye issue namba 5.

Na issue namba 5 inahusu deed.

Issue inasema hivi: Je, kutamka yale maneno yanayolalamikiwa ni kitendo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu?

Waheshimiwa Majaji, suala hili kwa lugha rahisi upande wa mashtaka wanasema kusema ni kitendo.

Ukitoa maneno ni kitendo.

Issue ni je, maneno ni matendo?

Waheshimiwa Majaji, hii confusion ya kusema maneno ni matendo ni ya kutengeneza kwa makusudi kwa upande wa mashitaka.

Ipo hivi, Waheshimiwa Majaji.

Kifungu cha 39(2)(d): “Any person who forms an intention to effect the intimidation to the executive...”

Masharti ya hicho kifungu lazima yadhihirishe kosa la uhaini kwa kuchapisha maandiko au udhihirishe kwa wazi.

Kwenye Kiingereza wamesema overt act or deed.

Kosa nililofanya ni kusema maneno.

Kwenye Khatibu Ghandi wamesema maneno matupu hayavunji mfupa.

Ndiyo maana wame-draft hati ya mashitaka kwa kusema kwamba mshtakiwa kwa kitendo chake cha kutamka, kwa sababu wangesema kwa kutamka kwake tu, Khatibu Ghandi ingewahusu.

Wanataka kuepuka kusema ni maneno.

Kwa mujibu wa hicho kifungu cha 39(2)(d), wametengeneza tofauti ambayo haipo ya overt act or deed.

Waheshimiwa Majaji, tuanze na haya maneno:

“What is overt act and what is deed?”

Waheshimiwa Majaji, hoja yangu ya kwanza ni act and deed ni their plain meaning means essentially the same things.

Kwa maana, Kiswahili chake cha wazi ni matendo.

Kwa Kiingereza, kwa mujibu wa Oxford Advanced Learner’s Dictionary, neno act limetafsiriwa kuwa “a particular thing that can be done”.

What is a deed? In the same Dictionary, deed is “a thing that somebody does”.

Inasema it is synonymous with an act. Therefore, a deed essentially the same thing as an act.

Ni kitu kilekile, kitendo.

Kifungu cha 39(2)(d) kinaposema kitendo cha uhaini kinapaswa kuthibitishwa na kitendo, not maneno.

Waheshimiwa Majaji, hayo maneno mawili, kuthibitisha, ni maneno mawili. Twende kwenye kamusi ya kisheria.

Black’s Law Dictionary, Seventh Edition.

What does it say?

“An act is something done or performed.”

Matumizi ya kawaida ni kitu fulani kinachofanywa.

Na imesema an act is also a deed.

Na inasema “it’s the process of doing or performing, it’s an occurrence...”

Ni matendo.

Waheshimiwa Majaji, kama an act is the same thing as deed, maneno hayawezi yakawa matendo.

Kwa hiyo, hiyo charge inayonikabili kwamba nimetenda uhaini kwa matendo yangu ya maneno, that’s nonsense.

Maneno hayawezi kuwa kitendo.

Kwa hiyo, charge itself on this particular point, it’s defective.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, nimetumia Oxford Dictionary na Black’s Law Dictionary kwa sababu moja tu.

Sheria yetu haijatafsiri hayo maneno.

Na kwa bahati mbaya sijapata case law ya hayo maneno.

Na wasaidizi wangu wanaonisaidia wanafanya kazi nzuri sana, Mungu awabariki.

Waheshimiwa Majaji, jana nilisema kwamba vyovyote mtakavyoamua, mtakuwa mmeweka historia.

Moja ya maeneo ya kusaidia ni kutoa muongozo for the future.

Mimi nimesema yote yana maana moja.

Information inasema kwamba “the accused person manifested his intention by deed altering”.

Wanafikiri wamezungumza uttering ya maneno lakini wameharibu kabisa hati yao ya mashitaka.

Unapotumia uttering, ujue unatumia neno la kisheria, si la mtaani.

Kifungu cha 5, Waheshimiwa Majaji, uttering includes or dealing with...

Ukitaka kujua kinazungumzwa kitu gani, nenda katika sheria yenyewe.

Ni matendo yanayohusiana na forgery, counterfeit.

Ngoja niwatafutie vifungu vyenyewe, Waheshimiwa Majaji.

Kifungu cha 342 cha sheria: Altering false documents.

Kifungu cha 343: Altering fake documents.

Kifungu cha 362: Altering metal into coins.

Walitaka kutumia neno altering la kwenye sheria ya Vyombo vya Habari kwenye Kanuni ya Adhabu.

Inawezekanaje?

Mimi nimeshitakiwa kwa mujibu wa Kanuni ya Adhabu.

Na kwa mujibu wa neno altering ya Kanuni ya Adhabu, altering ni forgery.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, shitaka hili ni bovu. Wameleta maneno ambayo hayapo kwenye sheria ya shitaka waliloleta.

Kwanza, altering si maneno.

Na pili, inaharibu uhalali wa shitaka lenyewe (destroys legal validity of information).

Waheshimiwa Majaji, the law now settles.

When charges introduces information that is new to the law.

Information inayoingiza maneno mapya katika sheria inabatilisha hiyo information.

Na haitibiki.

Nawapa authority ya Court of Appeal of Tanzania, Oswald Mangula vs Republic, 153 of 1993, Court of Appeal at Mbeya.

By Mr. Justice Samatta.

Kesi nyingine maarufu ni Musa Mwaikula vs Republic, 2009 TRL 387.

Nyingine, Waheshimiwa Majaji, ni Hassan Jumanne @ Msingwa vs Republic, No. 290 of 2014, Court of Appeal at Tabora.

Na kuna authorities nyingine nyingi ambazo zimetajwa.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, kwa introducing altering in information imeiharibu hiyo hati na haitibiki.

Waheshimiwa Majaji, to conclude on this point, the answer to the fifth issue must be NEGATIVE.

That is to say, number one, deed is not the same thing as spoken.

The second is hati ya mashitaka haitibiki, ni mbovu kwa namna ambayo haitibiki.

Mmeingiza maneno ya mtaani, maneno ambayo si ya kisheria, katika hati ya mashitaka.

Altering is not the same thing for the purpose of treason in section 39(2)(d).

Kwa ruhusa yenu, Waheshimiwa Majaji, mniruhusu nihamie hoja ya sita.

JAJI NDUNGURU: Muda uliobakia utatosha kumaliza hiyo hoja?

LISSU: Sitaimaliza, lakini ni vizuri nianze kwa muda uliobakia.

JAJI NDUNGURU: Kwa mtiririko mzuri, nadhani ungeanza kesho tu. Au mnasemaje upande wa mashtaka?

NASSORO KATUGA: Nasisi tunaona kwa mtiririko mzuri tuanze kesho. Kwa sababu tunaweza kurudi kesho akarudi upya.

JAJI NDUNGURU: Mshtakiwa, nadhani kesho unaweza kumaliza.

LISSU: Nafikiri naweza.

JAJI NDUNGURU: Utajielekeza yale unayozani ni ya muhimu.

LISSU: Nitajitahidi.

JAJI NDUNGURU: Shauri linahairishwa hadi kesho saa 3:00 asubuhi.

[Majaji wanatoka.]
 
Lissu alitakiwa kuwa full bright visiting professor vyuo vikuu vinavyoheshimika duniani akimwaga lectures na consultancies za sheria zilizoshindikana au zisizo na majibu duniani.
Kwanini hakuwahi Lecturer pale UDSM LLB? ilibidi awe pale anawa brush vijana.
 
Jamaa anauwasha Moto kweli kweli
 
Mpaka hapo tu, DDP alitakiwa kesho aseme hana haja ya kuendelea na kesi kuliko kupoteza muda wa siku 90 kufanya maamuzi.
 
Hv hapo kuna kitu samuya anaelewa hata kimoja kweli, au ni hii kariba takataka tu iliyombeba?!
 
Lissu is the best Tanzanian ever lived.
Mungu atamlinda kama alivyozuia risasi 16 zisiondoe uhai wake.
Amina.
 
Lissu anatusomesha bachelor ya sheria bila kulipia lakini kuna limtu linaitwa Mkunda na Wambura wakaa wanamshauri Bi Msumi huyo asitoke anyongwe atakata rufaa huko mbele.
Bi Msumi kwa kuwa darasa ana GPA ya 2.6 anawakubalia.
 
Hivi huko CCM hakuna hata mtu mmoja mwenye akili? Ona sasa mmeharibu hati ya mashtaka na kubatilisha kesi 💯! Kesi hii ni batili moja kwa moja. Ni mufulisi. Wapuuzi wakubwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…