Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Amosi Makalla amemshauri aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Iringa Mjini mchungaji Peter Msigwa ahamie CCM kufuatia sakata linaloendelea baada ya Msigwa kulalamikia kutotendewa haki kwenye Uchaguzi wa Uenyekiti wa CHADEMA Nyasa uliompa ushindi Sugu.
Akiongea Mkoani Arusha leo June 03,2024, Makalla amesema “Msigwa amesema ‘najitokeza hadharani kuwaeleza Watanzania na CHADEMA sisi muda wote tumehoji Tume ya Uchaguzi kumbe sisi ni Waongo hata sisi wenyewe hatufuati taratibu za uchaguzi Mimi nimeonewa nimeibiwa kura’ sasa na Mimi namuambia Msigwa pole sana Mchungaji njoo CCM ambako kuna demokrasia tele, kuna uwazi”
“Umeonewa pole sana Mchungaji Msigwa hicho Chama hakikufai tena njoo CCM, amesema tunawadanganya tu Watu kuhusu Katiba, Tume ya Uchaguzi kumbe Chama chetu hakifuati hata sheria za uchaguzi za Chama chake”
PIA SOMA
-
Kuelekea 2025 - Mchungaji Msigwa atangaza kukata rufaa kupinga Ushindi wa Joseph Mbilinyi (Sugu) Kanda ya Nyasa
-
Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa